MAELFU ya wananchi wa mkoa wa Mara
pamoja na mikoa jirani wakiongozwa na viongozi
wa Serikali,Dini na vyama vya Siasa wameuaga mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa
Mara John Gabriel Tupa aliyefariki juzi asubuhi akiwa wilayaniTarime kwa
shughuli za kikazi.
Akitoa salamu za rambirambi za Serikali mkoani Mara,Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Bartazal Kichinda alisema walipokea kwa masikitiko makubwa msiba wa ghafla wa mkuu wa mkoa wa Mara John
Gabriel Tupa kwa kuwa msiba huo umekuja
wakati mchango na usaidizi wa kiongozi
huyo ukiwa unahitajika zaidi mkoani Mara.
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA SHOMARI BINDA
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA SHOMARI BINDA
No comments:
Post a Comment