Mh. Naibu Meya Prosper Msofe ...Picha/Maktaba |
Siku
za hivi Karibuni Kumetokea Upotoshwaji kuhusu Madiwani wa Chadema na
Nafasi ya Naibu Meya kujihusisha na Biashara jambo ambalo si la kweli
hata kidogo.. soma Ukweli.
1. Kuna
upotoshwaji uliyofanywa na gazeti moja likidai kuwa Naibu Meya amejiingiza
katika biashara na kuchukua tenda ya kutengeneza Mabegi na Diari.
Jambo
hili ni la Uongo na Upotoshaji, inayoonyesha nia ya kumchafua Mh Naibu Meya
Prosper Msofe kwa nia ya kujenga taswira ya Chadema kutokuwa na viongozi makini.
Jambo hili si la Kweli kabisa na Ukweli ni Kwamba tenda ya Mabegi na Diari
ilitolewa kwa mujibu wa sheria na kupewa kwa kampuni ya Lewis Traders
inayomilikiwa na Lewis.
Tunaomba
wananchi na Wanachama wachadema waelewe kuwa hizo ni propaganda za watu
wachache wasiokitakia Chama Chetu cha Chadema Mema na kumtakia mema Kiongozi
wetu Naibu Meya Prosper Msofe. Naibu Meya ameonyesha kuwa Mchapakazi Hodari na
Mbunifu kwa muda mfupi aliyopata fursa Hiyo.
Tuendelee
kumuunga mkono Naibu Meya Mh. Proper Msofe kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa
tumekiunga mkono chama Chetu Chadema, ambayo ndio Tumaini pekee la Watanzania. Kwa ushahidi zaidi, hizi hapa Stakabadhi za malipo ya vifaa hivyo na kampuni inayofanya kazi hiyo:
2. Kuna
upotoshaji mkubwa uliofanywa na gazeti flani, likidai kuwa kuna
mgogoro wa kisiasa katika Madiwani wa Chadema Arusha Mjini, Jambo hili si la
kweli kabisa.
Ukweli
ni kwamba katika moja ya vikao vya madiwani wa Chadema Arusha mjini, kuliibuliwa
Hoja ya Kumchagua Mwenyekiti wa Madiwani mpya baada ya mjumbe huyo wa kikao
kueleza kuwa anaona kuwa viatu hivyo vimepaya kwa aliyevivaa sasa. Kimsingi
baadhi ya Madiwani wametathimini na kuona wanauhitaji wa kuwa na Mwenyekiti
Mpya kutokana na mtazamo wao mpya wa kukiimarisha chama.
Hivyo
baada ya kuibuka kwa hoja hiyo wajumbe walikubaliana kupanga siku mwafaka wa
kufanya Uchaguzi huo, kabla ya hilo kufanyika baadhi ya madiwani walitumiwa
barua kutoka ofisi ya Chadema wilaya ikiwataka madiwani hao kujieleza kardi
barua zilivyowataka.
Hakuna
mgogoro wala matusi yaliyoibuka kwenye kikao hicho , isipokuwa kumekuwa na kutofautiana kwa hoja,
2. Kuna changamoto inayojitokeza kwenye nafasi Mwenyekiti wa Madiwani wa sasa inaonekana kupwaya na uendeshaji wake wa majukumu kuwa si wakuridhisha, ambayo ilipelekea Madiwani kutamani kutumia Demokrasia yao kumpata kufanya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa madiwani wa Chadema.
Tukitumia uzoefu wa Bunge Kiongozi wa Kambi
ya Upinzani kuwa ndiye mwenyekiti wa Chama imejenga Heshima kubwa kwa Wabunge
wa Chadema ndani na nje ya Bunge.
Hivyo nao madiwani hao walitamani kuona
Kiongozi wa Madiwani anayeweza kuiletea Chadema heshima zaidi na kuweza
kuwaongoza Madiwani hao kwa Democrasia ya kweli na ni kwa uchaguzi tu ndio hilo
lingewezekana.
Kwa msingi huo kilichojitokeza ni Uitaji wa Demokrasia ya
kweli katika Madiwani wa Chadema Arusha Mjini, katika kutekeleza chama kuwa ni
cha Democrasia na Maendeleo.
Pia kuondoa dhana kuwa mtu akichaguliwa nafasi Fulani
akishinda kutekeleza majukumu yake kama ilivyoitajika hataondolewa. Ifahamike
kuwa Chadema ndio Chama pekee kinachoweza kukemea viongozi ake na hata
kuwawajibisha kwa kufuta Katiba na kanuni zilizoweka na Chama.
No comments:
Post a Comment