POLISI ASHINDA MILIONI 2 : ASKARI MWENYE BIDII YA KAZI, HASA USALAMA BARABARANI AMEJISHINDIA MILIONI 2 TASLIMU, JIJINI DAR ES SALAAM - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 13 March 2014

POLISI ASHINDA MILIONI 2 : ASKARI MWENYE BIDII YA KAZI, HASA USALAMA BARABARANI AMEJISHINDIA MILIONI 2 TASLIMU, JIJINI DAR ES SALAAM


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova(wa tatu toka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Askari wa usalama barabarani, Moses Alphage (wa pili kushoto) aliyeibu ka kidedea kwenye program ya kuhamasisha na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalam barabarani jijini Dar es salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio na kujishindia Sh 2 Milioni. Wa kwanza kushoto ni Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Albert Maneno na kulia ni mtangazaji wa Clouds Said Mohamed maarufu BONGE.
 Mfanyakazi wa Idara ya Masoko wa Kampuni ya Vodacom Albert Maneno (wa tatu kushoto) akiongea kabla ya kukabidhi Sh. 2 milioni kwa askari wa kikosi cha Usalama Barabarani Moses Alphage (wa kwanza kushoto) aliyeibuka kidedea katika program ya kuibua hamasa ya kazi kwa askari hao jijini Dar es Salaam iliyoendeshwa na kituo cha Redio Clouds FM. Fedha hizo zimetolewa na wafanyakazi wa Vodacom pamoja na wananchi mbalimbali walioguswa na programu hiyo. Wa kwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova.

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova akimkabidhi Askari wa usalama barabarani ,Moses Alphage fedha taslimu Sh. Milioni 2 zilizochangwa na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wasikilizaji wa kituo cha Redio Clouds FM kupitia program ya kuhamasisha na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalam barabarani jijini dar es salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio.
Askari wa usalama barabarani ,Moses Alphage,akiondoka zake kwa mwendo wa kikakamavu mara baada ya kukabidhiwa cheti na pesa taslimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 2 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova. Na Pamoja Pure Blog

No comments:

Post a Comment