Afisa
mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally
(Masoud kipanya) Akitoa ufafanuzi namna ya mchujo unavyo fanyika ili
kuwapata vijana na akina mama watakao ingia katika Maisha Plus/Mama
shujaa wa Chakula, Wakati wa kufanya zoezi la kuwachagua wale
watakaoingia katika kijiji cha Maisha Plus 2013/2014.
Majaji
wakuu walioteuliwa kwa ajili ya kufanya mchujo wa kuchagua Mama Shujaa
wa Chakula 30 na vijana 45 ambao baadae watafanyiwa usahili na kubakiza
wanawake 20 pamoja na vijana 30 kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda
na Burundi.
Afisa
mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally
(Masoud kipanya) aliyevaa kofia akipitia kwa umakini Fomu za mchujo za
Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus.
Wanafunzi 17 ambao wana fani mbalimbali na waliojitolea kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es salaam na Chuo kikuu cha Tumaini ambao wanawasaidia
majaji kupitia fomu za mchujo ili kuwapata wale watakaofanikiwa kuingia
katika Shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula
Baadhi ya wanachuo wakiwa wanaendelea kupitia Fomu kwa umakini kuhakikisha wanawatendea haki washiriki wote walioleta Fomu zao.
Mmoja
wa wanachuo akifanya maheesabu kwa makini ili kutoa alama kwa washiriki
walioleta fomu kwa ajili ya mchujo ya kuwapata watakaoingia katika
usahili wa Maisha Plus/ Mama shujaa wa Chakula
Baadhi ya Fomu zikiwa zimemalizika kupitiwa na wanafunzi wa Chuo kikuu ili kupelekwa kwa Majaji wakuu.
************
SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA/ MAISHA PLUS
- Fomu zaidi ya 4,000 za Mama Shujaa Maisha Plus zakusanywa
- Majaji 9 kusimamia zoezi la kuchaguwa wakulima wanawake 20 na vijana 45.
- Zoezi la kuchaguwa washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula na Maisha Plus limeanza leo ambapo zaidi ya fomu 4,000 zimekusanywa kutoka kwa washiriki.
Eluka Kibona, Meneja
Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akiongea wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo alisema
zoezi la kupitia fomu litachukuwa siku nne kuanzia Jumatatu tarehe 3 hadi
Alhamisi tarehe 6 Februari 2014.
Majaji
walioteuliwa wana kazi kubwa ya kupitia zaidi ya fomu 4,000 ambazo tumekishwazipokea
na nyingine bado zinawasili kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu. Baada ya
uchambuzi majaji watachaguwa wakulima wanawake 20 pamoja na vijana 45 ambao
watashiriki kwenye shindano la mwaka huu. Majaji watasaidia kuchambuwa fomu na
vijana 17 waliojitolea kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Jinsia.
“
Jopo la majaji linajumuisha
waliobobea kwenye masuala yanayohusu kilimo, ufugaji, usalama wa chakula, sera
na utetezi, uchumi, biashara, vyombo vya habari, vijana na maendeleo ya jamii.
Majaji ni
kama wafuatavyo:
Rose Tesha Meneja
Programu ya Maisha Salama shirika la VSO; Masoud Kipanya mwanzilishi wa shindano
la Maisha Plus; Tatu Abdi Juma mshindi wa tatu shindano la Mama Shujaa wa
Chakula 2012 ; Francis Bonda Mkurugenzi wa kampuni ya DMB na mwanzilishi
wa shindano la Maisha Plus, Edmund Matotay Mtafiti kutoka shirika la Oxfam; Anna Oloshoro mshiriki
wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula mwaka 2011; Carolyn Kandusi mtaalamu wa
jinsia kutoka shirika la PINGOS akitokea Loliondo; Zephaniah Mugittu mshauri
wa mnyororo wa thamani wa mboga mboga anafanya kazi na shirika la Oxfam akitokea
Lushoto, Tanga pamoja na Bernick Kimiro mshindi wa Maisha
Plus 2012.
Washiriki
wa Maisha Plus msimu huu ni vijana wa miaka 21-26 kutoka nchi za
Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda wanaogombania kitita cha
Fedha za kitanzania Milioni 25.
No comments:
Post a Comment