Afisa
Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama
akizungmza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro
juu ya umuhimu wa kujihusisha na kazi za Umoja wa Mataifa wakati wa
ziara za kutembelea shule mbalimbali za mkoa huo.
Na. Mwandishi wetu.
Vijana
wa shule za sekondari nchini wameaswa kuwa mabalozi wazuri pindi
watakapomaliza masomo yao juu ya kuhamasisha utekelezaji wa malengo ya
milenia kwa sababu ni dira ya maendelo ya taifa na dunia kwa ujumla.
Akizungumza
na wanafunzi wa shule ya Wasichana Kibosho, Lyamungo na Umbwe sekondari
hivi karibuni, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa,
Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema malengo ya milenia yanagusa Nyanja zote
za maendelo kwa vijana walio na wasio mashuleni.
Bi.
Nkhoma amewataka wanafunzi wafanye kazi za kujitolea na kuhakikisha
wanapeleka elimu waliopata kupitia vilabu vya Umoja wa Mataifa kwa jamii
na kuhamasisha dhana ya kujitolea kwa maslahi ya nchi.
“kila
ndani ya saa moja tuna vijana 50 ambao wanapata maambukizi ya VVU kati
ya miaka 14-24 ambao wengi kati ya hao ni Wasichana, hivyo msijihusishe
na masuala ya mapenzi mnapokuwa mashuleni”, amesema Bi. Nkhoma.
Bi.
Usia Nkhoma Ledama akionyesha takwimu za Mimba za Utotoni zilizotolewa
hivi karibuni (“Young People Today. Time to Act Now”) ambapo asilimia 25
ya watoto wa kike chini ya miaka 14 wanapata wakiwa mashuleni.
Pichani
juu na chini ni vijana wa shule ya Sekondari Umbwe wakifuatilia kwa
umakini mjadala wa masuala ya Umoja wa Mataifa uliiongozwa na Bi. Usia
Nkhoma Ledama (hayupo pichani).
Mwenyekiti
Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN)
Bw. Rahim Rajab Nasser akifafanua jambo kwa vijana waliojiunga na klabu
za Umoja wa Mataifa shuleni hapo juu ya umuhimu wa kuwa na cheti cha
klabu ya Umoja wa Mataifa
Msafara
wa wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na
wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN)
wakitazama baadhi ya kazi mbalimbali zinazofanywa na klabu ya Umoja wa
Mataifa katika shule ya sekondari Umbwe ikiwemo shughuli za kuchangia
damu, kusafisha mazingira na mengineyo yajihusishayo moja kwa moja na
shughuli za jamii.
"Ubovu
wa miundombinu ni changamoto kubwa kwa ziara yetu lakini ujumbe wa
shughuli za Umoja wa Mataifa lazima ziwafikie walengwa".
Afisa
Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama
akifurahia uwepo wake mbele ya wanafunzi wa Kibosho Girls shule ambayo
binafsi alisoma miaka 20 iliyopita, ambapo pia ujio wake ulikuwa chachu
na hamasa kubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Wasichana Kibosho wakimsikiliza kwa makini Bi. Usia Nkhoma Ledama.
Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama
akiwasisitizia wasichana wa shule ya Kibosho juu ya umuhimu wa kujiamini
na kujitambua wakati wa maamuzi yao binafsi.
Mmoja wa wanafunzi akiuliza swali kwa wajumbe wa Umoja wa Mataifa.
Kwa picha zaidi ingia hapa
No comments:
Post a Comment