TEKNOLOJIA : USHIRIKI WA TANZANIA KWENYE KONGANO LA TEHAMA LA DUNIA LA SHIRIKA LA USIMAMIZI WA MAWASILIANO DUNIANI ITU - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Friday, 22 November 2013

TEKNOLOJIA : USHIRIKI WA TANZANIA KWENYE KONGANO LA TEHAMA LA DUNIA LA SHIRIKA LA USIMAMIZI WA MAWASILIANO DUNIANI ITU

Timu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania katika Maonesho ya ITU Telecom World
Katibu Mkuu wa ITU ambalo ni Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani Dr. Hamadoun Toure akisikiliza Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Makame Mbarawa. Katikati ni Waziri wa ICT wa Thailand.
 ***********
Na Innocent Mungy - Bangkok Thailand
 
Tanzania inashiriki katika Kongano la TEHAMA la Dunia linaloandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani (ITU-International Telecommunications Union) linalofanyika katika jiji la Bangkok nchini Thailand.

Kongano hilo lenye Kauli Mbiu ya Kuchochea Mabadiliko Katika Ulimwengu wa TEHAMA, unashirikisha nchi wananchama wa ITU na wasio wanachama, Makampuni ya Mawasiliano Duniani, Taasisi na wasimamizi wa sekta ya Mawasiliano Pamoja na Serekali, wanashiriki Kongano hili katika kipindi ambacho mabadiliko makubwa katika Sekta ya Mawasiliano.

Mabadiliko haya yanapelekea dunia kuwa na Changamoto ya Kuyakubali Mabadiliko hayo na kukabiliana na Changamoto zake kwani faida za mabadiliko ni kubwa kwa Jamii Habari duniani. Akizungumza jijini Bangkok, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa amesema Tanzania iko tayari kwa na imeshapokea mabadiliko na imetekeleza mikakati ya kuhakikisha Tanzania inapokuwa mabadiliko bila tatizo.

Aidha Mheshimiwa Mbarawa amesema Tanzania inatambua umuhimu wa mabadiliko katika TEHAMA hususan kipindi hiki cha dijitali kwani ndio njia pekee ya kuharakisha maendeleo ya watanzania kwa ufanisi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma amesema Tanzania tayari  mstari wa mbele kuhakikisha inachochea mabadiliko ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili wananchi wafaidike na huduma za Mawasiliano. "Tuna mfumo mzuri wa usimamizi wa leseni za muingiliano wa teknolojia, sheria na kanuni nzuri ambazo zinawezesha mabadiliko katika TEHAMA kunufaisha watanzania. Tayari Tanzania imeingia katika mfumo wa Utangazaji wa digitali na tunaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuwepo kwa huduma nyingi zaidi kurahisisha maisha ya watanzania". Amesema Profesa Nkoma.

Taasisi kadhaa toka Tanzania zinashiriki Kongano hili kutoka Tanzania ikiwa ni pamoja na W ziara ya Afya, Kamisheni ya Sayansi na  Teknolojia,  DTBi ya wavumbuzi na wagunduzi, NICTBB inayosimamia mkongo wa Taifa, MaxCom.

Kongano hili linafanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 19 - 22 Novemba 2013. Tanzania inashiriki na kauli Mbiu ya nchi "Tanzania: Africa Strategic ICT Hub". Pamoja an Kongano pia yako Maonesho ya ICT yenye nia ya kuonesha jinsi nchi zinavyochochea maendeleo kwa raia wake kupitia TEHAMA. Banda la Maonesho la Tanzania limevutia watu wengi wanafikia kujifunza jinsi Tanzania imeweza kuchochea mabadiliko katika TEHAMA na jinsi wananchi wanafaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa nchini.

Aidha Baadhi ya Taasisi zinazoshiriki zinaangalia uwezekano wa kuchochea zaidi upatikanaji wa huduma zao kwa kuwa na washirika katika shughuli zao. Leo asubuhi Ujumbe wa Tanzania ulishiriki katika Mkutano Maalum wa Wawekezaji Katika Sekta ya Mawasiliano ulioendeshwa na Naibu Katibu Mkuu wa ITU Bwana Houlin Zhao.
 

No comments:

Post a Comment