Mgeni
Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa (katikati) akikata
utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Nembo Mpya ya PPF iliyoambatana na
Tovuti Mpya ya PPF.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa PPF,Dk. Aggrey
Mlimuka na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William
Erio.
Hivi ndivyo inavyoonekana Nembo Mpya ya PPF.
Nembo na Tovuti.
Bw. Bonda Nkinga akitoa Ushuhuda wake wake mbele ya
Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa
Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kuwasaidia watoto zake kusoma kupitia Fao la elimu.
Kijana
Peter William Mulokozi ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika
Shule ya Sekondari ya Mzumbe akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana na
Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF
ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Baba yake kupoteza maisha
ghafla.PPF ambao ni Mfuko pekee unaotoa fao la Elimu nchini endapo
Mwanachama anakuwa amefariki akiwa kwenye ajira.PPF imeweza kumsaidia
kijana huyu kusoma mpaka hapo alipofikia.
Kijana
Pascalia Nsatto ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha sita katika Shule ya
Sekondari ya Kimataifa ya Moshi akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana
na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF
ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Wazazi wake wote wawili
kupoteza maisha. Kwa Picha zaidi Bofya Hapa >>>
No comments:
Post a Comment