![]() |
"Nimeshinda kesi tena! Kwa kweli Mungu anatupenda sana na tutaendelea kupambana kutafuta haki bila hofu. Miili yetu na nafsi zetu zimepoteza maumivu kwa sababu ya mateso yaliyojaa uongi na hila. Hata hivyo tutaendelea na kelele za kupigania haki bila kurudi nyuma huku uvumilivu ukiwa nguzo yetu kuu" alisema Mbunge Lema , katika viwanja vya Mahakama Kuu Arusha mara baada ya kushinda kesi dhidi yake na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo zikihusisha kilichodaiwa kuwa uchochezi kwa wanafunzi wa Uhasibu Arusha wamzomee Mulongo na kufanya fujo... Kesi hiyo imefutiliwa mbali baada ya washitaki kuomba hivyo pamoja na kwamba leo ndio ilikuwa siku ya kuanza kusikiliza ushahidi wa Mkuu wa Mkoa, Dean of Students, Makamu Mkuu wa Chuo na Maofisa wa Polisi wakiongozwa na OCD Muroto. Kwa hisani ya Seria Tumainiel (SeriaMtoto WikiLiks Tumainiel) |
WAZIRI WA NISHATI MHE. NDEJEMBI AZINDUA RASMI MITA JANJA
-
*Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja
(smart meter) yenye lengo la kuboresha na kumrahisishia mteja kufanya
manun...
6 hours ago

No comments:
Post a Comment