Mbunge Kabati akikabidhi msaada wa vitabu vya masomo mbali mbali kwa wakuu wa shule za sekondari jimbo la Iringa mjini
Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Bw. Francis Godwin akipokea msaada wa kompyuta kutoka kwa mbunge Ritta Kabati. |
MBUNGE
wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ametimiza ahadi yake
ya madawati 100,vitabu kwa shule za msingi na sekondari
pamoja na kompyuta moja kwa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Iringa (IPC)
Akikabidhi
ahadi hiyo jana kabati alisema kuwa amelazimika kutimiza ahadi
hiyo ili kupunguza sehemu ya ahadi mbali mbali ambazo alipata
kuwaahidi wananchi wa jimbo la Iringa mjini pamoja na zile ambazo
aliombwa na wanahabari mkoa wa Iringa ili kusaidia kuongeza
vitendea kazi kwa ofisi ya wanahabari mkoani hapa.
Kabati
alisema kuwa madawati hayo 100 aliyokabidhi ni kwa shule za msingi
nane za jimbo la Iringa mjini na vitabu ni kwa ajili ya shule za
sekondari 5 za jimbo la Iringa mjini.
Mbunge huyo alisema madawati hayo yanathamani ya
zaidi ya Tsh milioni 6 wakati vitabu hivyo ameviomba kutoka kwa
wadau wake kwa ajili ya kusaidia kupunguza uhaba wa kiada na ziada
katika shule za sekondari jimbo la Iringa mjini.
Hata
hivyo alisema kuwa misaada hiyo amekuwa akiitoa mfukoni mwake na
posho yake anayoipata bungeni hasa ukizingatia yeye si mbunge wa
jimbo ambae anapewa bajeti ya
kusaidia maendeleo ya jimbo kwa maana ya mfuko wa maendeleo wa jimbo
.
"
Mimi nimekuwa nikitumia posho zangu kusaidia maendeleo jimbo la
Iringa mjini hasa mkitambua kuwa mimi sina mfuko wa jimbo ila kama
ningelikuwa mbunge wa jimbo kero hizi zingetatuliwa kupitia mfuko
wa jimbo.....ila bado nahawakikishieni nitaendelea kuchangia
maendeleo ya jimbo la Iringa mjini"
Akielezea
juu ya msaada wake wa kompyuta kwa aliyoikabidhi kwa uongozi wa IPC
Kabati alisema kuwa mbali ya msaada huo wa Kompyuta bado
ataendelea kuwasaidia wanahabari Iringa ikiwa ni pamoja na kumwomba
waziri wa habari , vijana utamaduni na michezo Dr Fenella Mkangala
ili ikiwezekano IPC kuendelea kusaidia zaidi hasa kupitia IPC
Vicoba mpango ambao umekuwa ukiwasaidia wanahabari kupata mikopo
nafuu
Kwa
upande wake mlezi wa IPC Salim Asas alimshukuru mbunge Kabati kwa
kuendelea kuwasaidia wanahabari na jamii nzima ya jimbo la Iringa.
Alisema kuwa kinachofanywa na mbunge Kabati kinapaswa kuigwa na
wabunge wengine katika kuwasaidia wanahabari ila jamii inayowazunguka pia. Picha na habari na Francis Godwin.
No comments:
Post a Comment