DKT. JAKAYA KIKWETE AZINDUA AWAMU YA NNE YA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI BAHARINI, JIJINI DAR - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 26 October 2013

DKT. JAKAYA KIKWETE AZINDUA AWAMU YA NNE YA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI BAHARINI, JIJINI DAR

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuashiria Uzinduzi wa Mkutano wa Nne wa Kugawa Vitalu vya Utafutaji Mafuta na Gesi Baharini katika Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Professa Sospeter Muhongo na kulia pembeni ya Rais ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi Joyce Kisamo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye Mkutano wa Nne wa Kugawa Vitalu vya Utafutaji Mafuta na Gesi Baharini katika Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe walihudhuria uzinduzi wa Mkutano wa Nne wa Kugawa Vitalu vya Utafutaji Mafuta na Gesi Baharini katika Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwaeleza waandishi wa habari jinsi utafiti wa Gesi na mafuta unavyofanyika baharini muda mfupi baada ya kuzindua awamu ya nne ya Utafiti wa Gesi na mafuta uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete aliwahi kuingoza wizara ya Nishati na Madini.Picha na Freddy Maro.

No comments:

Post a Comment