MKE WA RAIS WA TANZANIA MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA CHUO CHA MONMOUTH, NEW JERSEY MAREKANI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Sept 2013

MKE WA RAIS WA TANZANIA MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA CHUO CHA MONMOUTH, NEW JERSEY MAREKANI

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth kilichoko huko New Jersey nchini Marekani mara tu baada ya kuwasili chuoni hapo tarehe 24.9.2013. Mama Salma yupo nchini Marekani akifuatana na Rais Jakaya Kikwete anayehudhuria Mkutano wa 68 wa Umoja wa Mataifa unaofanyika New York.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongoza kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. Mama Salma Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.
 .  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea katika kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea vitabu kutoka kwa Dkt. Edward Christensen, Vice President for Information Management. Chuo Kikuu hicho kilitoa zaidi ya vitabu  4000 kwa ajili ya Tanzania. Wengine wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni pamoja na Waziri wa Afya Dr. Hussein Mwinyi na Makamu Rais wa Chuo Bwana Sarsar na Mwishi ni nBwana John McLaughlin. Picha na John Lukuwi, Kwa Picha zaidi Bofya hapa>>>

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad