Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.) akisalimiana na Naibu Waziri wa Uingereza anayeshughulikia Mambo
ya Nje na Jumuiya ya madola, mhe. Mark Simmonds walipokutana kwa
mazungumzo Mjini New York wakati wa Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja
wa Mataifa.
Ujumbe ulioambatana na Mhe. Simmonds. |
Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Simmonds kuhusu masuala ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. |
Ujumbe
wa Tanzania wakati wa mazungumzo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya
Ulaya na Amerika, Balozi Dora Msechu, akifuatiwa na Bi. Tully Mwaipopo,
Bw. Grayson Ishengoma na Bw. Togolani Mavura Maafisa wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Picha na habari na Rosemary Malale, New York
|
Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)
ameishukukuru na kuipongeza Serikali ya Uingereza kwa kuanzisha huduma
mpya itakayowawezesha Watanzania kupata viza za kuingia nchini humo kwa
haraka.
Huduma
hiyo ambayo ilitangazwa na nchi hiyo hivi karibuni kupitia Balozi wa
Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Diana Melrose ni moja ya mipango ya nchi
hiyo ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili. Huduma hiyo
hukamilika kwa takribani siku tano hadi kupata viza.
Akizungumza
hivi karibuni na Naibu Waziri wa Uingereza anayeshughulikia Mambo ya
Nje na Jumuiya ya Madola, Mhe. Mark Simmonds Mjini New York, Marekani
wakati wa Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mhe. Membe
alisema kuwa anaishukuru nchi hiyo kwa kuichagua Tanzania katika mpango
huo ikiwa ni mshirika wake muhimu wa maendeleo na kwa kuzingatia kuwa
uchumi wa Tanzania unakua kwa haraka katika siku za hivi karibuni hivyo
itarahisisha na kuimarisha biashara baina ya nchi hizi mbili.
Aidha,
Mhe. Membe aliongeza kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakijishighulisha na
biashara mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo Uingereza hivyo mpango
huo wa viza za haraka utawasaidia kuimarisha biashara zao badala ya
kukatishwa tamaa na mlolongo mrefu wa kufuatilia viza uliokuwepo hapo
awali.
“Tunaishukuru
sana Serikali ya Uingereza kwa kuanzisha huduma hiyo ya utoaji viza za
haraka, hata hivyo bado tunaiomba ifikirie tena uwezekano wa kurejesha
huduma ya utoaji viza Jijini Dar es Salaam badala ya kufuatilia viza
hizo Nairobi nchini Kenya”, alisema Waziri Membe.
Aidha,
aliomba kiwango cha nyongeza kilichowekwa cha shilingi laki mbili na
nusu kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa viza hiyo ya haraka kipunguzwe
kwani ni kikubwa kwa Watanzania.
Akizungumza kwa
upande wake, Mhe. Simmonds alisema kuwa Uingereza itaendelea kuimarisha
ushirikiano na Tanzania hususan katika masuala ya biashara na
uwekezaji.
Mkutano
huo wa Mhe. Waziri Membe na Mhe. Simmonds ulihudhuriwa na Wajumbe
wengine akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu.
No comments:
Post a Comment