Msanii
mahiri wa Kughani Mashairi kwa mtindo wa kisasa kabisa,Mrisho mpoto
akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma na vitongoji
vyake waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya kamata Fursa
twendzetu,iliofanyika ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma. Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group,imekwishafanyika
mikoa zaidi ya mitano ikiwemo Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara, Mbeya,Iringa
sambamba na mkoa wa Dodoma,ambamo semina hizo zote zimeonesha mafanikio
makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
Sehemu ya washiriki wa semina hiyo ilipokuwa ikiendelea...
Wakifuatilia
kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo ya
kamata fursa twendzetu,mkoani Dodoma.
Mwakilishi
wa NSSF-Makao Makuu,Salim Khalfan akifafanua masuala mbalimbali
yatokanayo na faida za kujiunga na shirika hilo la NSS,ndani ya semina
ya kamata fursa twendzetu iliofanyika kwenye moja ya ukumbi
wa hotel ya Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Sehemu ya ya watu wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo.
Meneja
wa NSSF mkoani Dodoma,Bwa.Kirondera Nyabuyenze akizungumza fursa
mbalimbali zitokanazo na shirika la NSSF,Nyabuyenze amewataka watu
mbalimbali wajitokeze kwa wingi kujiunga na NSSF,ili kujipatia fursa
mbalimbali zikiwemo mikopo,matibabu na mambo mengine mbalimbali.
Mwakilishi
wa Kampuni ya Maxmalipo,Renard Munuri akizungumza kwenye semina ya
Kamata Fursa Twenzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali
yanayofanywa na kampuni yake katika kusaidia huduma za jamii,ndani ya
moja ya ukumbi wa hotel ya Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa
Dodoma.
Mmoja wa Watangazaji mahiri wa
Clouds FM Millard Ayo,akizungumzia fursa mbalimbali alizokumbana nazo na namna
alivyozifanyia kati na kujipatia sehemu ya mafanikio katika kupambana na
maisha.
Baadhi
ya wasanii ambao wamenufaika mara baada ya kujiunga na Shirika la
NSSF,shoto ni Queen Doreen na Mwasiti wakijadiliana jambo na mdau
Phillip,wakati semina ya Kamata fursa twendzetu ilipokuwa
ikiendelea.
Sehemu ya wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza mapema kwenye semina ya fursa kwa vijana
Sehemu ya meza kuu ya watoayo mada wakishangilia jambo.
PICHA ZAIDI BOFYA <<HAPA>>>.
No comments:
Post a Comment