TCRA YATOA SHUKRANI KWA BLOGGERS NA ADMIN WA MITANDAO MBALI MBALI KWA KUHAMASISHA KAMPENI YA "FUTA DELETE KABISA" - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 21 August 2013

TCRA YATOA SHUKRANI KWA BLOGGERS NA ADMIN WA MITANDAO MBALI MBALI KWA KUHAMASISHA KAMPENI YA "FUTA DELETE KABISA"


Tunashukuru Bloggers wote na Admin wa Facebook groups pamoja na Online Forums mbalimbali kuunga mkono kampeni ya FUTA DELETE KABISA.
Kama ambavyo tumesema mara nyingi nia ya kampeni si kuingilia uhuru wa kutoa mawazo yetu bali tunashauri matumizi mazuri. Tunapinga matusi, uongo, post za kuumiza wengine, uchochezi na uchonganishi.

Tunasisitiza watumiaji kulinda staha zao kwa kuweka picha zisizo mbaya, kulinda watoto, kutoweka picha za udhalililishaji kwa wanawake, Watoto au ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki.

Kabla ya ku-share post tafakari na tumia uhuru huu vizuri. Tusitumie vidole vyetu kuvuruga amani, kutukanana au kuchafua watu.

Mungu ibariki Tanzania!

No comments:

Post a Comment