Mh Lema akishuhudia jeneza lenye mwili wa marehemu likipakiwa garini tayari kwa safari
Mbunge akiwa na sura ya huzuni kwa kuondokewa na kijana wake mpambanaji
Gari ya chama iliyobeba jeneza la mwili wa marehemu likiondoka viwanja vya Hospitali ya Mt Meru kuelekea Usa River.
Mwenyekiti
wa Vijana Chadema na Katibu wa Chadema Arumeru Mashariki, Bw Methew
Kishili akimuelekeza jambo Mbunge Lema katika viwanja vya hopsitali ya
Mt Meru wakisubiri mwili wa marehemu.
Msafara
ukiondoka hospitalini hapo kuelekea Usar River ambapo misa ya kumuaga
marehemu na kutoa heshima za mwisho itafanyika kabla ya safari ya
kuelekea Morogoro. Mh Lema na Mh Nassari pamoja na viongozi wengine wa
Chama Mkoa na Wilaya ya Arumeru watashiriki katika ibada hiyo na zoezi
la kuaga mwili wa marehemu.
Mh
Lema na Mh Nassari wakiwa nyumbani kwa marehemu katika zoezi la kuaga
mwili kabla ya safari ya kuelekea Morogoro. Wengine waliokaa ni Bw
Alphonce Mawazo na Joseph Moses kulia kabisa.
ENZI ZA UHAI WAKE
Hapa
ni enzi za uhai wake akiwa eneo la Mahakama Kuu Jijini Arusha (mwenye
t-shirt ya M4C) na watunza amani na usalama wenzake wa chama katika moja
ya kesi za Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema. Marehemu ameacha
mke na watoto watatu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi,
Amina! Kwa picha zaidi bofya hapa>>>
No comments:
Post a Comment