DKT. GHARIB BILAL APOKEA MAANDAMANO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA VIKUNDI VYA MTANDAO WA WAKULIMA WA TANZANIA (MVUWATA) MJINI MOROGORO - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


27 Jul 2013

DKT. GHARIB BILAL APOKEA MAANDAMANO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA VIKUNDI VYA MTANDAO WA WAKULIMA WA TANZANIA (MVUWATA) MJINI MOROGORO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, mmoja kati ya wachangiaji bora wa kuendeleza Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) Justice Shekilango, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika ,Julai 26, 2013 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wasanii wa kikundi cha ngoma ya Muhembe cha mjini Dodoma, wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wakulima wa Jumuiya ya Mtandao wa Wakulima wa Tanzania (MVUWATA) wakiwasili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa maandamano wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo, yaliyopokelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanamtandao wa Jumuiya ya wakulima wa Tanzania (MVUWATA) baada ya kupokea rasmi maandamano ya wakulima ya maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Picha na OMR.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad