DR. GHARIB BILAL APOKEA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA WATOTO WA HALAIKI KUTOKA NMB - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

3 May 2013

DR. GHARIB BILAL APOKEA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA WATOTO WA HALAIKI KUTOKA NMB


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea sehemu ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. Milioni 35, kwa ajili ya vijana wa Haraiki ya Mbio za Mwenge utakaowashwa Visiwani Pemba Mei 6, mwaka huu, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Domina Feruzi, wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa benki hiyo, Elieza Msuya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wageni wake kutoka Benki ya NMB, baada ya makabidhiano ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. milioni 35 kwa ajili ya vijana wa Haraiki wa mbio za Mwenge unaotarajia kuwashwa Mei 6, mwaka huu Visiwani Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Domina Feruzi (wa pili kulia) Meneja wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa benki hiyo, Elieza Msuya (kulia) Ofisa Mahusiano wa benki hiyo, Doris Kilale (wa pili kushoto) na Huruma Mwaihomba, Ofisa Mahusiano wa benki hiyo, baada ya makabidhiano hayo.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633