JUMLA ya wanariadha
wapatao 300 wameshathibitisha kushiriki mbio za kumbukumbu za kifo cha hayati
Waziri Mkuu na mpambanaji wa uhuru wa nchi hii, Edward Moringe Sokoine ambazo
zinatarajiwa kufanyika Aprili 12 wilayani Monduli, Mkoani Arusha.

Wanariadha kutoka
katika mikoa ya, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Dar es salaam na Arusha
wameshathibitisha kushirki katika mbio hizo za kwanza kufanyika katika historia
ya nchi hii tangu uhuru.
Hayo yamebainishwa na
mratibu wa mbio hizo ambaye pia ndiye mwongozaji wa mbio hizo, Wilhelm
Gidabuday akizungumza na TAIFA LETU.com, kwa njia ya simu kutoka Dar es salaam na
kusema kwamba tayari kupitia ofisi za chama cha Riadha mkoa Arusha (ARAA), wamethibitisha
kushiriki mbio hizo.

Gidabuday alisema kuwa
kujitokeza kwa wanariadha hao ni ishara nzuri kwani pamoja na kwamba ndio mara
ya kwanza, kwa muitikio huo, wanatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 500.
“Tumeshapata maombi
kutoka kwa wanariadha kutoka katika mikoa mbalimbali tofauti na Arusha,
kutokana na Taarifa ya ARAA, tayari kuna idadi ya wanariadha mia tatu,
tunatarajia kuwa na wakimbiaji zaidi ya mia tano,” alisema Gidabuday.
Kuhusu zoezi la
usajili, Gidabuday alisema kuwa zoezi hilo litaanza mapema baada ya sikuukuu za
Pasaka kumalizika na kuongeza kuwa zoezi hilo litafanyikia katika Ofisi za
ARAA, zilizoko katika uwanja wa mpira wa miguu wa Sheikh amri Abeid jijini
Arusha kwa ada ya sh. 2000 za Tanzania.

Mbio hizo za umbali wa Kilomita 10 na kilomita
2 kutembea na kukimbia maandalizi yake kwa mujibu wa Waratibu wake mpaka sasa
zimeshafikia hatua nzuri na kwa mujibu wa Waratibu wake, hatua zinazofanyika ni
kufanya mazungumzo na Mgeni Rasmi ambaye kuna uwezekano akawa mmoja wa viongozi
wakuu wa taifa hili. Kwa hisani ya Taifa Letu.com
Wote tutajaa huko Monduli siku hiyo, hata iweje tutajaa mwanangu.
ReplyDelete