KWA mujibu wa mashuhuda wa ajali iliyotokea leo asubuhi Jijini
Arusha, inakadiriwa zaidi ya watu 18 wamepoteza maisha kufuatia
kufukiwa na gema la mchanga/moram wakati wakichimba na kupakia kwenye
malori.
Ajali hiyo mbaya imetokea katika machimbo ya moram nje
kidogo ya Jiji eneo jirani na Moshono-Kiserian ambapo vijana hao
wanaokadiriwa kufikia idadi hiyo walikuwa wakipakia moram kwenye magari
mawili, moja ni Fuso na lingine kubwa zaidi (tani 18) na yote mawili
yamefukiwa kabisa na kifusi.
Shuhuda mmoja wa ajali ambae pia ni
mchimbaji ameieleza Blog hii kwamba kwa kawaida gari ndogo kama Fuso
hupakiwa na watu 7, na hiyo kubwa huwa na watu 12 bila kuhesabu dereva
na utingo.
Blog hii iliweza kushuhudia sehemu ndogo sana ya Fuso
ikionekana lakini gari nyingine ilikua imefukiwa kabisa na kupondeka
vibaya.
Miongoni wa waliofikwa na mauti ni pamoja na madereva wa
magari hayo. taarifa za eneo la tukio zinaeleza utingo mmoja ameokolewa
akiwa amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali lakini dereva wake
amefariki dunia.
Katika eneo la ajali hali ni ya simanzi na vilio
toka kwa kina mama huku baadhi wa wababa na marafiki na ndugu wa jamaa
waliofukiwa wakishindwa kujizuia na kuangua kilio.
Meya wa
Manispaa Mh Gaudence Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless
Lema ni miongoni mwa viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana
na kikosi cha Jeshi la Wananchi kufanya uokozi.
Blogu hii
ilishuhudia pia Wachina wakipeleka moja ya mashine zao (Excavator)
kuongeza nguvu katika kusaidia kufukua miili ya watu hao iliyonaswa na
kifusi hicho.
Jeshi la wananchi likiendelea na uokozi . kwa picha zaidi ya matukio hayo Bofya hapa >>>
No comments:
Post a Comment