Mhe. James Mbatia awasilisha hoja Binafsi Bungeni kuhusu udhaifu wa Elimu Tanzania - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 1 February 2013

Mhe. James Mbatia awasilisha hoja Binafsi Bungeni kuhusu udhaifu wa Elimu Tanzania


 Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo  Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki (katikati) pamoja na Mbunge wa Viti maalumu  Ester Bulaya, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, leo.
 Mwanasheria Mkuu Mkuu wa Serikali Mh. Jaji Frederick Werema (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Wazir wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla, leo Bungeni mjini Dodoma.
 Waziri  wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe (kulia) akizungumza na   Mbunge wa Korogwe Mjini, Yusuph Abdallah Nassir, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, leo.
 Mbunge wa Iramba Magharibi Mwingulu Nchemba (kulia) akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Joshua Nasari, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, leo.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa (kushoto), Mbunge wa Viti Maalumu, Margaret Sitta (wa pili kushoto) na Waziri wa fedha William Mgimwa (mwenye miwani) pamoja na Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia (kulia) wakibadilisha mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo ,  baada ya Mbunge  James Mbatia kuwaslisha hoja yake binafsi kuhusu Udhaifu uliopo katika sekta ya Elimu nchini.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, akionyesha kimoja kati ya vitabu vinavyotumika mashuleni alipokuwa akijibu hoja mbalimbali  zinazohusu elimu baada ya Mbunge wa kuteuliwa wa  NCCR- Mageuzi, James Mbatia, kuwakilisha hoja yake binafsi ya Udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini. Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment