Tamasha la viazi
linafanyika katika mji mkuu wa Sudan , Khartoum, kwa lengo la
kuwahamasisha watu kula na kulima zaidi viazi .
Maharagwe, wali , mihogo na nafaka nyingine vimekuwa vyakula vikuu zaidi kuliko viazi nchini Sudan na maeneo mengine ya Afrika Zaidi ya vyakula sitini vilivyoandaliwa kwa viazi vitaandaliwa katika tamasha hilo kuwawezesha watu kuonja.
Kutakuwa pia na maonyesho ya mbinu za ukulima wa viazi na namna ya kuvihifadhi .
Waandalizi wa mkutano huo wanasema kuwa Sudan inaweza kuwa mzalishaji mkuu wa viazi barani Afrika kutokana na hali yake ya hewa na raslimali kubwa ya ardhi.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment