MKE WA FILBERT BAYI AMFUATILIA MWANARIADHA MAARUFU WILHELM GIDABUDAY -JIJINI ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 28 December 2012

MKE WA FILBERT BAYI AMFUATILIA MWANARIADHA MAARUFU WILHELM GIDABUDAY -JIJINI ARUSHA


Willhelm Gidabuday


HABARI NYEPESI YA KUFUNGA MWAKA: Mama Bayi leo amenifwatilia kwa nyuma kwa kutumia gari la FRANCIS JOHN (aliyekuwa Rais wa RT), Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na GERALD SOLOMON BABU. Mama alikuwa amekaa ktk passenger side huku kwa nyuma alikuwa amekaa FABIAN JOSEPH. Mimi nilikuwa nikiongozana na ROGARTH JOHN na mzee WADE wa Arusha.

Story ikawa hivi:

MAMA BAYI: Gida vipi,
MIMI: Safi shikamoo mam...a,
MAMA BAYI: Malapa yako sasa utayasemea wapi?,
MIMI: Mungu anajua,
MAMA BAYI: Wewe una Mungu?,
MIMI: Mungu yupo; Heri ya mwaka mpya,
MAMA BAYI: Kwako mwaka mpya umefika?,

Mimi sikuthubutu kumjibu mama wa watu vibaya maana najua yeye bado ni mama mzazi hata ingekuwa vipi!!. Ila nilishangazwa na kiwango cha hasira alizonkuwa nazo kiasi kwamba sasa ni dhahiri kwamba yeye na mumewe walikuwa wameifanya TOC kuwa mali yao. Lakini najiuliza kwani Bayi kashindwa nini hadi kunitumia mkewe?

Kabla ya kunifikia alikwenda kuhakikisha sehemu zote ambazo huwa ninafanya shughuli zangu, kitendo kinachoashiria kwamba kuna mchoro ambao anauchora!!.

Pamoja na hayo HERI YA MWAKA MPYA WADAU WOTE WA MICHEZO NA WATANZANIA WOTE.

By Gidabuday.


Haya yalitokea mitaa ya Mzunguko wa mnara wa Mwenge,eneo la Azimio la Arusha. 
Mbali na hayo Gidabuday alifanya mahojiano na blog hii, kuwa yeye ana mikakati mikubwa sana hapa nchini ya kuinua huu mchezo wa Riadha kutoka ngazi ya chini hadi kimataifa. Pia amesema baada ya Sikukuu za krismas na mwaka mpya Mungu akipenda anatarajia kufanya jambo moja la kihistoria ambalo hata TOC hawaja wahi kulifanya ,ila amesema ni mapema mno kulisema.

1 comment:

  1. Yaliyosemwa na huyo kamanda inaonekana ni ya kweli kabisa, ndio maana hata mke wa meja Bayi anaingilia kimafia. Lakini alichoshindwa mzee mama ataweza?. Na ikitokea Buda buda anapatwa na tatizo lolote sisi tutamfuatilia mama na mzee wake Kimara hadi Kibaha.

    ReplyDelete