Na Mussa Juma, Arusha -JUMLA ya wanafunzi 6,838 waliofaulu mtihani wa darasa la saba
mwaka huu, mkoani Arusha, wamekosa nafasi ya kujiunga na masomo ya
Sekondari kutokana na uhaba wa nyumba vya madarasa 172 .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Evelyine Itanisa
alitoa taarifa hiyo, juzi katika kikao cha kamati ya uchaguzi wa
wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2013 mkoani Arusha.
Itanisa alisema wanafunzi hao, wanatoka katika
halmashauri sita za mkoa Arusha na ni halmashauri moja tu ya Karatu
ambayo imeweza kuwachukua wanafunzi wote waliofaulu mwaka huu.
Alisema katika jiji la Arusha wanafunzi 2420
wamekosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa 61, Ngorongoro
wanafunzi 441 wamekosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba 11.
Alisema Halmashauri ya Arusha vijijini
wanafunzi 1880 wameshindwa kujiunga na sekondari kutokana na uhaba wa
vyumba 47.
“Pia Halmashauri ya Longido kuna wanafunzi 140
ambao wanahitaji madarasa manne, Meru wanafunzi 1,159 wakiwa na mahitaji
ya vyumba 29, wilaya ya Monduli wanafunzi 807 wamekosa nafasi kutokana
na kukosekana madarasa 20”alisema Itanisa.
Alisema kutokana na hali hiyo, ameziagiza
halmashauri hizo sita za mkoa wa Arusha kuiga mfano wa halmashauri ya
Karatu, kwa kuhakikisha zinajenga vyumba vya madarasa vya kutosha ili
kuhakikisha wanafuzi wote waliofaulu wanapata nafasi.
“Ili kuhakikisha watoto waliofaulu wote
wanaendelea na sekondari, kila halmashauri inapaswa ihakikishe
inakamilisha ujenzi wa madarasa kabla ya februari mwakani “alisema
Itanisa.
Hata hivyo, Katibu Tawala huyo alisema kiwango cha
ufaulu kwa Mkoa wa Arusha, kimekuwa kikipanda kwa miaka mitatu sasa
mfululizo ambapo mwaka huu jumla ya wanafunzi 26,464 wamefaulu mitihani
kati ya wanafunzi 37,493 waliofanya mitihani.
“Matokeo haya yanafanya Mkoa wa Arusha uwe
umefaulisha kwa asilimia 70.6 na waliofaulu ni wavulana 12,608 na
wasichana 13,856”alisema Itanisa.
|
JAFO AIPONGEZA TBS KWA KUANDAA TUZO ZA UBORA KWA WAFANYABIASHARA NA
WAJASIRIAMALI
-
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Selemani Jafo (Mb) ametoa rai kwa
Wazalishaji wa bidhaa Nchini kuweka kipaumbele suala la ubora wa bidhaa
kwani ndio aje...
54 minutes ago
No comments:
Post a Comment