Hoteli
ya Girafee Ocen View iliofungiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Terezya Huvisa wakati alipotembelea leo katika mfululizo wa ziara
ya kukagua hali ya Mazingira kwenye fukwe za Bahari.
Uchafu katika Ufukwe wa Hoteli ya Girafee Ocen View.
Lulu Mussa na Ali Meja - Ofisi ya Makamu wa Rais
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais – Mazingira Dk. Terezya Huvisa hii leo ameendelea na
ziara ya kikazi ya kukagua hali ya mazingira katika hoteli zilizopo
pembezoni mwa fuke za bahari ya hindi, jijini Dar es Salaam.
Ziara ya leo imeanzia katika hotel
ya Giraffe Ocean View, na katika hali ya kushangaza maagizo aliyotoa
Naibu Waziri Charles Kitwanga katika hoteli hiyo mapema mwezi huu ya
kurekebisha mfumo wa majitaka na kuweka fukwe katika hali ya usafi
hayajazingatiwa.
Hatua kali zimechukuwa wa Hotel
hiyo ikiwa ni pamoja na kufungiwa mpaka hapo itakapotimiza masharti
yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004. “Naifunga
Hotel hii ya Girafee mpaka hapo itakapotimiza masharti ya hifadhi ya
mazingira” alilisitiza Dkt. Huvisa.
Sambamba na hilo Waziri Huvisa
ameipongeza Hotel ya Beach Comber kwa kuwa na mkakati endelevu wa mfumo
wa maji taka na hifadhi ya fukwe kwa ujumla. Dkt. Huvisa amesema kuwa
zoezi hilo ni mkakati endelevu wa kukagua hoteli zote na viwanda, Ofisi
ya Makamu wa Rais – Idara ya Mazingira kwa kushirikiana na Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wanafanya kazi hiyo
kwa kikamilifu.
Kwa mujibu wa sheria ya Mazingira
ya mwaka 2004, Hoteli na Viwanda vyote vilivyoanzishwa kabla ya matumizi
ya sheria hiyo vinatakiwa kufanya (Environmental Audit) na baada ya
sheria ya Mazingira hutakiwa kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira
(Environmental Impact Assessment).
Katika ziara ya siku mbili
iliyofanywa na Waziri Huvisa pamoja na Naibu wake Charles Kitwanga
imepelekea kuchukua hatua kali za kisheria ambapo Hotel ya Double Tree
na Giraffe Ocean View zimefungiwa mpaka hapo zitakotimiza masharti
waliyopewa.
No comments:
Post a Comment