Dr. Raisi
Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi katika maadhimisho ya siku ya
Ukimwi Duniani yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu Mjini Lindi, huku
wadau mbalimbali wa masuala ya mapambano ya ukimwi wakishiriki kwa
kufanya maonyesho na kutoa elimu na maelezo mbalimbali yanayohusu
mapambano ya ukimwi, Rais Pia ameshuhudia utiwaji saini wa msaada wa
Dola za Kimarekani Milioni 308 kutoka mfuko wa Global Fund uliosainiwa
kati ya Katibu katibu wa Ofisi ya rais Paniel Lyimo na Ramadhan
Kijahkati Kabu Mkuu Wizara ya Fedha huku Mfuko wa Global Fund
ukiwakilishwa na Christoph Benn Mkurugenzi wa mfuko huo.
Christoph
Benn Mkurugenzi wa mfuko Global Fund akizungumza wakati wa maadhimisho
ya siku ya Ukimwi Duniani iliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu mjini
Lindi.
Rais
Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya wananchi wa mkoa wa Lindi wakati
wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani iliyofanyika mjini Lindi leo .
kutoka kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi wa Tume ya
kudhibiti Ukimwi TACAIDS Fatuma Mrisho na kushoto ni mkuu wa mkoa wa
Lindi Ludovick Mwananzila
Rais
Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya wananchi wa mkoa wa Lindi wakati
wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani iliyofanyika mjini Lindi leo .
kutoka kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Hussein Mwinyi, Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi
TACAIDS,Fatuma Mrisho.
Rais
Jakaya Kikwete akishuhudia Utiwaji wa Saini wa msaada wa dola za
Kimarekani milioni 308 kwa ajili ya mapambano ya Ukimwi nchini, mkataba
huo umesainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Paniel Lyimo kushoto na
Ramadhan Kijah katikati, kulia ni Christoph Benn mkurugenzi wa Mfuko wa
Global Fund, waliosimama nyuma kushoto ni Mkewa Rasi Mama Salma Kikwete,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na kulia ni Ursula
Muller Mjumbe wa bodi ya The Global Fund.
Rais
Jakaya Kikwete akiongozana na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiingia kwenye
uwanja wa Ilulu mjini Lindi tayari kwa kushiriki katika maadhimisho ya
siku ya ukimwi Duniani ambayo yamefanyika mkoani Lindi kitaifa.kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa TACAIDS Fatma Mrisho na Mkuu wa Mkoa wa Lindi
Ludovick Mwananzila
Rais
Jakaya Kikwete akimuonyesha jambo Mkurugenzi wa tume ya kudhibiti
Ukimwi Fatma Mrisho wakati alipotembelea mabanda mbalimbali katika
maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani mjini Lindi leo.
Rais
Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Bw.Rajab Mwenda afisa masoko
wa Mpango wa damu Salama wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye
maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani mjini Lindi leo.
Baadhi
ya viongozi wa Dini na waalikwa mbalimbali waliohudhuria wakifuatilia kwa karibu matukio yaliyokuwa yakiendelea
katika maadhimisho hayo.
Mwakilishi
wa mfuko wa bima ya Afya ya Jamii mjini Lindi NHIF Bi. Fortunata
Raymond wa tatu kutoka kulia akiongoza maandamano ya wafanyakazi wa
mfuko huo katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani.
Kikundi cha matarumbeta kikiongoza maandamano yakipita mbele ya Rais kwenye uwanja wa Ilulu leo mjini Lindi.
Kikundi
cha kuigiza kutoka mfuko wa bima ya afya ya Jamiii NHIF kikiwapa ujumbe
kwa wananchi wa mkoa wa Lindi kuhusu maambukizi ya ukimwi.
No comments:
Post a Comment