Na mwandishi Wetu, Charles Ngereza ( www.charlesngereza.blogspot.com)
WATU zaidi
ya mia moja katika kijiji Cha Ngabobo Wilayani Arumeru , Mkoani Arusha;
hawana mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa na mvua kubwa
iliyoambatana na upepo mkali katika eneo hilo.
Wakizungumza
na waandishi wa habari wananchi hao walisema kuwa mvua hizo zilinyesha kwa muda
wa nusu saa na kuangusha mamia ya miti ,kubomoa na kuharibu barabara na kusababisha
mawasiliano katika eneo hilo kuwa magumu.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho Zabulon Kimaki alisema
kuwa tukio la limeacha kaya zaidi ya ishirini zenye watu mia moja na thelathini
zikiwa hazina mahali pa kuishi.
“Hali ilikuwa ya kushutua sana ,mvua hiyo
ilikuwa sio ya kawaida lakini kibaya limesababisha watu takariban mia moja na
ishirini kulala nje kutoakana na mabati ya nyumba zao kuezuliwa na
upepo,hawajaweza hata kuokoa kpande cha bati na hatujui yalipo mapaa na bati
zilizoezuliwa na upepo”alisema Kimaki.
Alisema kuwa
watoto zaidi ya themanini wameshindwa kwenda shule kufuatia tukio hilo
kusababisha kupoteza ama kuharibiwa vifaa vya shule kama vile madaftari ,vitabu na sare za shule kusombwa
na maji.
Alisema
serikali inapaswa kuwapelekea huduma za kijamii wananchi hao ikiwemo mahema na
chakula ili kuweza kuwasaidia kukabili hali waliyo nayo kwa sasa.
“Uongozi wa
halmashauri ulifika jana hapa kungalia madhara yaliyotokea lakini hawajatoa
chochote ila tunamshukuru Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari
kwa kutoa chakula ambacho kitawasaidia
wahanga hawa kujikimu kwa siku
chache”alisema Kimaki.
Mmoja wa
wahanga wa tukio hilo Sambeke Saiteru alisema kuwa kwa sasa wanalala nje pamoja
na familia yake hali ambayo imefanya watoto wake kuanza kuumwa kifua kuitokana
na baridi kali nyakati za usiku.
Alieleza
kuwa licha ya upepo kuezua paa la nyumba yake lakini pia maji yaliyotririka kwa
wingi yaliingia ndani na kusomba vyakula na vyombo vya nyumbani na sasa kubaki
bila chochote.
“Hapa nilipo
nimebaki na nguo nilizovaa toka siku ya tukio ,hata watoto wangu saba nao
hawana mavazi maji ya mvua ilisomba kila kitu hapa nyumbani,tungefurahi kupata
msaada wa haraka kutoka serikalini”alisema Saiteru.
Alisema kuwa
tukio hilo limeacha hofu katika familia yake kwani lilitokea wakiwa ndani ya
nyumba yao .
Mwananchi mwingine Edward Ngoiyo alisema tukio hilo pia lilitokea
akiwa na familia yake ndani ya nyumba ambapo alisema alishangaa kuona paa lote
likipigwa na upepo na kuondolewa na kuchwa wakinyeshewa.
“Watoto
wangu walichanganganyikiwa ,hali ilikuwa ni ya kutisha ,tumepoteza nguo vitabu
vya watoto na wa kwangu wawili wameshindwa kwenda shule kutokana na janga
hili”alisema Ngoiyo.
Alisema kuwa
kwa sasa anaishi na familia yake katika zizi la ngombe hali ambayo inaendelea
kuhatarisha maisha yake na familia aliyo
nayo.
Alisema kuwa
halmshauri walifika na Mbunge na kutoa msaada wa chakula kwa waathirika kwa kila mmoja kupata kilo
mbili za mchele na sukari kilo moja.
“Tunaomba
wafanye haraka kutuokoa katika hali hii ,hatukutarajia imetokea kwa kasi na
ghafla na kufanya halii hii tuliyo nayo”alisema Ngoiyo.
Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kusema kuwa tayari uongozi wa halimashauri ya Meru umekwishafika katika eneo
la tukio kufanya tathmini ya madhra yaliyotokea.
“Ni kweli
tukio limetokea ila mimi niko safarini ila nimekwisha agiza uongozi wa halmashauri kwenda katika eneo la tukio kufanya tathmini
na kutoa msaada unaohitajika lakini pia Mbunge Joshua Nassari alifika na kutoa
msaada wa chakula ”alisema Munasa.
Alisema katika
timu hiyo ya halimashauri wapo watu wanaohusikama masuala ya maafa na wahandisi
wa ujenzi wa halaimashauri hiyo.
|
No comments:
Post a Comment