Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata Kaaya Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa),
kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo hicho mwaka 2010 kwa Kutambua
mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini. Sherehe
hiyo fupi ilifanyika leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata
Kaaya akisoma risala kabla ya kumkabidhi Rais Kikwete Cheti cha Udaktari
wa Public Health (Honoris Causa),
kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo Desemba mwaka 2010 kwa Kutambua
mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu na Waziri wa Ardhi
Prof. Anna Tibaijuka, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Hussein
Mwinyi na viongozi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili baada ya kukabidhiwa Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa),
kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo hicho mwaka 2010 kwa Kutambua
mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini leo .
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata
maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha
Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Wizara ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba leo, Ikulu jijini Dar es salaam.
********
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete leo Ijumaa Novemba 23, 2012 amepokea taarifa ya
maendeleo ya ujenzi wa Kampasi mbili za tiba ya afya vinavyojengwa
katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Mloganzila huko Kisarawe, ambavyo pia
vitatumika kama hospitali hapa nchini.
Kwanza
Rais amepokea maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha
Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba .
Ujenzi wa kampasi hii umeshaanza na kufikia hatua ya juu na hospitali inatarajiwa kuanza shughuli zake rasmi mwaka 2015.
Kulingana
na Bw. Humba, maandalizi ya kufanikisha uanzishaji wa Chuo/ Hospitali
hiyo vimeshaanza ambapo baadhi ya wataalamu wakiwemo Madaktari na
watumishi wengine wako nchini na nje ya nchi kwa ajili ya masomo na
mafunzo mbalimbali.
Chuo
hicho kinatarajia kuwa na vifaa vya kisasa vya tiba vinavyokidhi
mahitaji ya Afya na Elimu ya Udaktari wa kiwango cha Kimataifa.
Rais
pia amepokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Mloganzila
ambapo katika ujenzi na uanzishwaji wa Kampasi hizi zote, Rais Kikwete
amesimamia kuanzia hatua za awali.
Kampasi
ya Mloganzila ambayo ni sehemu ya Hospitali kuu ya Muhimbili inajengwa
kwenye eneo la ekari 3800 na itakua sehemu ya kutolea mafunzo kwa
wanafunzi wa udaktari na huduma za Afya, lakini pia itakua sehemu ya
kutolea matibabu ya maradhi yote makuu na ya kawaida nchini.
Ujenzi
wa Hospitali hii unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari, 2013 na
unatarajiwa kukamilika miaka miwili baada ya ujenzi.
Katika
hafla hiyo Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
Prof. Ephata Kaaya ametumia nafasi hiyo kumkabidhi Rais Kikwete Cheti
cha Udaktari wa Public Health
(Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Afya
na Sayansi Shirikishi, Muhimbili Disemba, 2010 kwa Kutambua mchango wa
Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini.
Akitoa
taarifa hiyo ya maendeleo kwa Rais Kikwete, Prof. Kaaya amesema tayari
wataalamu na wafanyakazi wanaotarajiwa kufanya kazi katika kampasi ya
Mloganzila wameshaanza mafunzo. Mara hospitali hiyo kubwa na ya kisasa
itakapokamilika itakua na uwezo wa vitanda vya kulaza wagonjwa mia sita
(600).
Rais
Kikwete amewapongeza wataalamu wote kwa juhudi zao na kuwa ahidi kuwa
lengo lake ni kuhakikisha nchi inaondokana na adha ya kupeleka wagonjwa
nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Rais
amesema moja ya lengo kubwa la serikali yake, ni kutoa kipaumbele
katika sekta ya Afya ili kuhaklikisha watanzania wanapata huduma bora,
kupanua mafunzo ya Afya na kuongeza wataalamu watakaoweza kutibu
magonjwa yote makubwa hapa hapa nchini.
Rais
amewaahidi watendaji wa Kampasi zote mbili kuwa atahakikisha ujenzi wa
huduma hizi muhimu kwa Umma haukwami kwa sababu ya ukosefu wa pesa kwani
ni jambo ambalo amedhamiria.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-DSM
23 Novemba, 2012
No comments:
Post a Comment