Rais JAkaya Mrisho Kikwete akipeana
mkono na Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu.
Wengine ni Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha
New Ford Kenya, Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru
Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha TNA. Kushoto kwa Rais
ni Wengine ni (kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA Bi Rachel
Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda
(kushoto) na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe
huo Ikulu jijini Dar es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana
mkono na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru
Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha TNA. Kushoto kwa Rais ni
Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford
Kenya. Wengine ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu
(kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA Bi Rachel Shebesh, na
Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda (kushoto) na mbunge
wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe huo Ikulu jijini Dar
es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya. Kulia kwake Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha TNA. Kushoto kwa Rais ni Wengine
ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu
(kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA Bi Rachel Shebesh, na
Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda (kushoto) na mbunge
wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru
Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha TNA, Waziri wa Sheria wa
Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya, Naibu Waziri wa
Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu (kulia), Mbunge wa
kuteuliwa wa chama cha TNA Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa
tiketi ya TNA Moses ole Sakuda (kushoto) na mbunge wa zamani Mhe
Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam
Jumapili Oktoba 21, 2012 .Picha na IKULU
--
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametaka wananchi wa
Kenya wapewe nafasi ya kuamua ni viongozi gani wanawataka katika Uchaguzi Mkuu
uliopangwa kufanyika Machi mwakani.
Aidha,
Rais Kikwete amesema kuwa wananchi wa Kenya wanayo haki ya msingi kabisa kuamua
hatma ya taifa lao katika Uchaguzi Mkuu huo.
Mheshimiwa
Rais aliyasema hayo Oktoba 21, 2012 alipokutana na kufanya mazungumzo na
ujumbe wa wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya nchini Kenya uliomtembelea
Ikulu jijini Dar es salaam.
Ujumbe
huo uliongozwa na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru
Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa
chama cha TNA na Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama
cha New Ford Kenya. Wote wawili ni wagombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi
ujao.
Wengine
katika msafara huo walikuwa ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe.
Kambi Kazungu, Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa
tiketi ya TNA Moses ole Sakuda na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli.
Rais
Kikwete aliwapongeza kwa kuamua kufanya kazi kwa pamoja licha ya kuwa
watakuwa washindani katika
kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu huo.
Mheshimiwa
Rais ameitakia heri nchi ya Kenya katika uchaguzi huo ujao, na kusisitiza
kwamba nchi hiyo ya jirani ina umuhimu katika mustakabali wa kiuchumi kwa
nchi za Afrika Mashariki.
Rais
Kikwete wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) alikuwa miongoni
mwa viongozi walioshughulika sana kutafuta ufumbuzi wa ghasia na vurugu
zilizozuka kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya.
Rais
Kikwete alikaa siku tatu nchini Kenya akitafuta usuluhishi wa vurugu hiyo ya
kisiasa nchini humo, ambayo katika mazungumzo yake leo ameyataja kama ajali
iliyolipata Taifa la Kenya, na ambayo majirani wake hawaitarajii kutokea katika
uchaguzi ujao.
Mwisho
Imetolewa na:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
DAR ES SALAAM,
21 Oktoba, 2012
No comments:
Post a Comment