MWILI WA KAMANDA LIBERATUS BARLOW WAAGWA JIJINI MWANZA LEO - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 15 October 2012

MWILI WA KAMANDA LIBERATUS BARLOW WAAGWA JIJINI MWANZA LEO


Msafara wa magari ya kuleta mwili wa marehemu Liberatus Barlow yakiingia katika uwanja wa Nyamagana.
  Maaskari walioteuliwa kubeba mwili wa marehemu Liberatus Barlow wakiwa wamejipanga vyema ili mwili uweze kutolewa ndani ya gari ili uwekwe sehemu nzuri ambayo kila mtu anaweza kuuaga vizuri.
  Hapa wakiushusha kutoka ndani ya gari ili waweze kuubeba.
Safari ya kuelekea sehemu maalum iliyopangwa kwa ajili ya mwili wa marehemu ilianza hiviii..

Afande George Msangi akiongoza ratiba za kumuaga aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Liberatus Ballow aliyeuawa usiku wa kuamkia jumamosi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi katika eneo la Kitangiri karibu na Hotel ya Tai Five.
Viongozi mbalimbali wa Kiserikali wakisimama kwa dakika chache kuupa heshima mwili wa marehemu kamanda Liberatus Barlow.
Afisa Usalama wa Taifa Meja Jacob Mutashi mwenye suti nyeusi kulia akionekana pichani.
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Polisi wakionekana na huzuni
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Everest Ndikillo akienda kuuaga mwili wa marehemu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow katika uwanja wa Nyamagana leo.
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Kaminishina Manumba akisalimia na Mkuu wa Wilaya ya Magu Bi. Jackline Wana huku Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza Bi. Rosemary Mwanyika akiwa mbele mwenye suti nyeusi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Joyce Masunga akiweka saini katika daftari la maombolezo katika msiba wa marehemu kamanda Liberatus Barlow katika uwanja wa Nyamagana.
Wakuu wa wilaya mbalimbali katika Mkoa wa Mwanza na baadhi ya viongozi wa serikali, vyama vya kisiasa wakionekana katika picha wakiwa na majonzi makubwa kumpoteza kamanda Liberatus Barlow.
Wanafamilia wa marehemu kamanda Liberatus Ballow wakiwa na majonzi makubwa sana katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili wa mpendwa wao Liberatus Barlow.
Wananchi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Mwanza na nje ya Mkoa wa Mwanza wakionekana katika tukio la kuuaga mwili wa Kamanda Liberatus Barlow.
Maafisa wa Majeshi aina mbalimbali kutoka Tanzania wakionekana katika hafla la kuuaga mwili wa marehemu kamanda Liberatus Barlow.
Umati mkubwa watu wakiwa katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Liberatus Barlow. Picha zote na BPlus

No comments:

Post a Comment