Msanii wa filamu Cloud naye akichangia mawazo yake wakati wa semina hiyo.
Pichani
Juu na Chini ni Meneja wa MNET Ukanda wa Afrika Mashariki Bi. Risper
Muthamia wakati wa kutangaza rasmi kutolewa kwa Africa Magic Viewers
Choices Awards (AMVCA), ambapo amesema zitawashirikisha Wasanii,
Waandaji na Waandishi wa Filamu kutoka Barani Afrika zitakazofanyika
Lagos nchini Nigeria tarehe 9 Machi 2013.
Bi. Risper Muthamia amesema kuwa Filamu
zote zilizotengenezwa kwa ajili ya Televisheni na mfululizo wa vipindi
vya Luninga (Series) zinaweza kuwasilishwa kuwania tuzo hizo iwapo
zilitengenezwa na kurushwa hewani au kuonyeshwa hadharani katika kipindi
cha kati ya May 1, 2011 hadi April 30, 2012.
Aidha amefafanua kuwa Filamu au vipindi
vitakavyoshiriki katika tuzo hizo viwe ni katika lugha ama ya
Kiingereza, Hausa (Nigeria), Swahili au Yoruba na kusisitiza kuwa hakuna
Lugha nyingine itakayokubalika.
Ameongeza kuwa Filamu na Sinema
zilizotengenezwa kwa ajili ya Televisheni zinapaswa kuwa na urefu wa
kati ya Dakika 60 mpaka 90 wakati Mfululizo wa vipindi vya Luninga
(Series) ni kwa muda wa dakika 30 mpaka 60. Wasanii wamekumbushwa kuwa
ili kuweza kushiriki katika tuzo hizo wanapaswa kuwasilisha nakala 6 za
DVD za filamu zao.
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania
Barbara Kambogi akizungumza katika semina fupi ya wadau wa tasnia ya
Filamu nchini pamoja na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa wasanii
watakaopelekea kazi zao wahakikishe kuwa sio za kuiga na zina hati
halali ya kusajiliwa na COSOTA.
Msanii wa filamu nchini almaarufu kama
Mtitu akitoa maoni yake kuhusiana na tuzo AMVCA zilizoanishwa na Africa
Magic kwa kushirikiana na Multichoice kwa ajili ya kutambua mchango wa
wasanii wa bara la Afrika kwa lengo la kukuza sekta ya filamu Kimataifa.
Wasanii wa filamu wakisimama kwa dakika
moja kumkumbuka Aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Tanzania na Afrika
kwa Ujumla aliyefariki dunia ghafla Marehemu Steven Kanumba.
Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini
(TAFF) Bw. Simon Mwakifamba akiwasisitiza wasanii na watengenezaji wa
filamu kuhakikisha zinakuwa na maudhui ya Kiafrika na ubora
unaokubalika.Bw. Mwakifamba amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa
kupenda filamu za nyumbani na kushiriki katika kuzipigia kura pindi
zinapokuwa katika mashindano ya aina mbalimbali kama itakavyokuwa katika
Africa Magic Viewers Choice Awards (AMVCA).
Meneja wa MNET Ukanda wa Afrika
Mashariki Bi. Risper Muthamia akielezea kuwa taarifa zaidi kuhusiana na
tuzo hizo zinapatikana katika tovuti ya Africa Magic ambayo ni www.africamagic.tv
na kuwa kiingilio cha kushiriki katika tuzo hizo ni bure na mwisho wa
kuwasilisha fomu za ushiriki ni Oktoba 31, 2012. Kulia ni Meneja Masoko
wa Multichoice Tanzania Furaha Samalu.
Baadhi ya wasanii wa filamu nchini
waliohudhu8ria semina fupi iliyohusiana na Africa Magic Viewers Choice
Awards (AMVCA). Kutoka kushoto ni Msanii Sajuki akiwa amembatana na
mkewe na msanii nguli Dkt. Cheni.
Mchekeshaji na Msanii wa Filamu Steven Nyerere akitoa maoni yake kuhusiana na tuzo hizo.
Meneja Masoko wa Mutichoice Tannzania
Bi. Furaha Samalu sambamba na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Barbara
Kambogi (wa kwanza kulia).
Yusuf Mlela na msanii mwenzake.
Msanii nguli katika sanaa ya maigizo na filamu hapa nchini almaarufu kama Bi. Mwenda.
Charles Baba naye alikuwepo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps
Entertainment Bw. Jai (wa pili kushoto) ambao ni wasambazaji wa filamu
nchini akizungumza na maafisa wa kampuni ya Multichoice.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Bi. Furaha Samalu akibadilishana mawazo na msanii wa Filamu nchini maarufu kama Cloud.
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania
Barbara Kambogi akiteta jambo na mmoja wa washiriki wa semina hiyo
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufafanua vigezo
vitakavyotumika wakati Africa Magic Viewers Awards (AMVCA)
zinazotarajiwa kufanyika March 9, 2013 Lagos Nigeria.
No comments:
Post a Comment