Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amesema kuwa atabuni tume ya uchunguzi baada ya polisi kuwafyatulia risasi maelfu ya wafanyikazi wa migodi waliogoma siku ya Alhamisi.
Wanawake na watoto wakienda kutafuta habari za waume zao kwenye mgomo huko Rustenburg, Afrika Kusini
Polisi wanasema watu thelathini na wanne waliuwawa katika tukio hilo.
Rais wa chama cha wafanyakazi ambacho siyo rasmi, Joseph Mathunjwa, wa Association of Mineworkers and Construction Union, aliiambia BBC kuwa wanataka tume huru ya kimataifa kuchunguza mauaji hayo kwa sababu chama chake tayari kinalaumiwa kwa ghasia hizo.
Kampuni inayomiliki migodi hiyo, Lonmin, imeahidi kusaidia familia za walioathirika, lakini inashikilia kuwa mgomo huo haukuwa halali.
Chama hicho kinataka nyongeza ya mshahara wa zaidi ya dola 1,000 kwa mwezi.
Watu kumi wakiwemo polisi wawili waliuwawa kabla ya tukio la siku ya Alhamisi.
No comments:
Post a Comment