Mwendesha Mashtaka Mkuu mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya kukabiliana na Uhalifu wa Kivita ameapishwa mjini Hague.
Bi Fatou Bensouda, aliyekuwa wakati mmoja Waziri
wa Haki nchini Gambia,ndiye Mwafrika na pia mwanamke wa kwanza
kushikilia cheo hicho.
Mojawapo wa wajibu wake wa mwanzo ni kumleta
Hague mwana wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muamar Gaddafi, Saif
al-Islam Gadaffi, ambaye ameshtakiwa kwa makosa dhidi ya binadamu na
wakati huohuo kuongoza mashtaka yanayomkabili aliyekuwa kiongozi wa
Ivory Coast, Laurant Gbagbo.
Fatou Bensouda amechukua nafasi ya mtangulizi
wake ambaye aliyeondoka, Luis Moreno Ocampo, ambaye ameongoza mahakama
hiyo kwa zaidi ya mwongo mmoja.
No comments:
Post a Comment