Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika
akitoka nje ya viwanja vya Bunge la Tanzania mapema leo mjini Dodoma.
Mbunge
wa Jimbo la Ubungo John Mnyika akiteta na Mbunge wa jimbo la Wawi Hamad
Rashid Mohamed
(kushoto) na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo mara baada ya
kuondolewa Bungeni mapema leo mjini Dodoma.
unaoendelea.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dodoma
---------
MSIMAMO WA MBUNGE WA UBUNGO(CHADEMA)JOHN MNYIKA JUU YA KAULI YAKE BUNGENI LEO
-
Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu
kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais
Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi
Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye
Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa
Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa
bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye
ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba.
Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu
mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa
bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza
Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe
marekebisho!
John Mnyika(MB)
19 Juni 2012
No comments:
Post a Comment