Wafuasi wa Muslim Brotherhood
watafanya maandamano makubwa kote nchini Misri kupinga hatua ya baraza
la kijeshi la nchi hiyo kujilimbikizia madaraka.
Mwishoni mwa wiki iliyopita wakuu wa jeshi la
Misri walitangaza amri ya kuvunjwa kwa bunge na halafu kijitwika
madaraka ya bunge hilo.
Hii leo Jumanne wabunge ambao wengi wao ni wafuasi wa Muslim Brotherhood wanatarajiwa kujaribu kuingia bungeni kwa nguvu.
Na wakati kura za urais zingali zinahesabiwa,wagumbezi wote wawili wamedai kupata ushindi.
Mohammed Mursi, ambae ni kiongozi wa chama cha
Brotherhood's Freedom and Justice Party (FJP), siku ya jumatatu
alitangaza kwamba amepata jumla ya asilimia 52 ya kura zilizopigwa siku
ya Jumapili.
Bwana Mursi aliahidi kushirikiana na Wa-Misri
wote kuhakikisha kuna maisha bora, uhuru zaidi, demokrasia na amani
imedumishwa kote nchini.
Lakini wasimamizi wa kampeni ya Bwana Ahmed
Shafiq ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa mwisho wa Misri amedai kuwa yeye
ndie mshindi wa kura hizo na wafuasi wa Muslim Brotherhood waliwatisha
wapiga kura.
Hata hivyo vyombo vya habari vya kitaifa pamoja
na waangalizi huru wa kura hizo wanaamini kuwa Bwana Mursi ameshinda
uchaguzi huo kwa zaidi ya asilimia tatu au nne ambayo ni zaidi ya kura
milioni moja.
Inaonekana kwamba baraza kuu la kijeshi la Misri
linaamini kwamba Bwana Mursi ndie ataibuka mshinda hivyo basi
ikatangaza amri ya kupunguza uwezo na mamlaka ya rais.
No comments:
Post a Comment