Wakuu wa Mikoa na Wilaya watembelea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


27 May 2012

Wakuu wa Mikoa na Wilaya watembelea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)


Baadhi ya Wakuu Wa Mikoa na Wilaya walipotembelea Jengo jipya la Utawala la Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).
 Naibu Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Mipango, Utawala na Fedha Prof. Shaban Mlacha (Katikati) Akitoa Maelezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliotembelea Chuo katika Maonyesho yaliyohusisha wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma.
 Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakiwa katika Picha ya Pamoja Mbele ya Jengo la Utawala Mpya wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).
a Michoro ilichorwa na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ambazo leo wamepata nafasi ya kuonyesha kazi zao tofauti na masomo wanayosomea.
Baadhi ya wakuu wa Mikoa na Wilaya wakiwasili katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuoni Hapa wakati wa maonyesho ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakisalimiana na wenyeji wao wakati walipokuja kwenye maonyesho ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ambapo wanafunzi waliweza kuonyesha uwezo wao tofauti na masomo wanayosomea
Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akitoa maelezo kwa baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa waliokuja Kuona kazi za wanafunzi wa UDOM wakati wanafunzi hao Wakionyesha Uwezo tofauti na Masomo wanayosomea
Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliweza pia kupata nafasi ya kutembelea Jengo la Utawala la Chuo Kikuu Cha Dodoma na kufanya ziara ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakati walipokuja Kuangalia maonyesho ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu Cha Dodoma.


Picha na LJ Media Company

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad