Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda Apokea Msaada wa Vifaa vya Kutolea Huduma za Afya Zikiwemo Dawa za Kutibu Ugonjwa wa Kichocho na Maabara Ndogo za Kubaini Dawa Zilizotengenezwa Chini ya Kiwango (Dawa Feki) - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


27 Feb 2012

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda Apokea Msaada wa Vifaa vya Kutolea Huduma za Afya Zikiwemo Dawa za Kutibu Ugonjwa wa Kichocho na Maabara Ndogo za Kubaini Dawa Zilizotengenezwa Chini ya Kiwango (Dawa Feki)

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda (wa pili kushoto) akipokea msaada wa vifaa vya kutolea huduma za afya zikiwemo dawa za kutibu ugonjwa wa kichocho na maabara ndogo za kubaini dawa zilizotengenezwa chini ya kiwango (dawa feki) kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Ujerumani ya MERCK inayoshughulika na utengenezaji wa dawa za binadamu,vifaa tiba na kemikali Dkt.Karl-Ludwig Kley leo jijini Dar es salaam. Vifaa hivyo vitasambazwa katika hospitali mbalimbali nchini na vituo vya afya vilivyo mipakani
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda(katikati) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Dkt. Peter Mmbuja wakifuatilia maelezo ya kitabu cha mwongozo wa maabara ndogo inayohamishika ya kubaini dawa zilizotengenezwa chini ya kiwango (dawa feki) yaliyokuwa yakitolewa na balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus-Peter Brandes.
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus-Peter Brandes (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda juu ya dawa zilizotolewa leo jijini Dar es salaam na kampuni ya Ujerumani ya MERCK inayoshughulika na utengenezaji wa dawa za binadamu,vifaa tiba na kemikali.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Dkt. Peter Mmbuji.
 Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad