Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akijadili jambo na Spika wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Mninwa Mahalangu (Mb) ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Utendaji CPA Afrika alipofika nchini kuhudhuria Mkutano wa siku moja wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa) unaofanyika mjini Arusha tarehe 25 Februari, 2012.
Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimkaribisha Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana (Mb) Mjini Arusha, mara alipofika nchini kuhudhuria Mkutano wa siku moja wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madolakanda ya Afrika (CPA Africa) unaofanyika mjini Arusha. Mhe. Rose Mukandabana ni Rais wa Chama hicho kwa kanda ya Afrika.
Wajumbe wa sekretariati ya Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madolakanda ya Afrika (CPA Africa), wakiwa katika kikao cha kamati ya utendaji ya chama hicho kilichofanyika mjini Arusha. Kutoka kulia ni Dk. Thomas Kashililah, Katibu wa Kanda wa chama hicho ambae pia ni katibu wa Bunge la Tanzania, Demetrius Mgalami, Naibu katibu wa CPA Afrika na Said Yakubu Mjumbe wa Sekretariati ya CPA Afrika.
Katibu wa Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa) Dk. Thomas Kashililah ambaye pia ni katibu wa Bunge la Tanzania akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Mninwa Mahalangu (Mb) (Kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Utendaji CPA Afrika wakati wa kikao cha kamati ya Uongozi ya chama hicho iliyokutana Mjini Arusha, leo. Picha na Owen Mwandumbya
No comments:
Post a Comment