VODACOM FOUNDATION YAKARABATI KITUO CHA POLISI MTO WA MBU KWA MARA YA KWANZA TANGIA KIJENGWE MWAKA 1967 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


24 Feb 2012

VODACOM FOUNDATION YAKARABATI KITUO CHA POLISI MTO WA MBU KWA MARA YA KWANZA TANGIA KIJENGWE MWAKA 1967



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC).Thobias Andengenye akipanda mti wa ukumbusho wa uzinduzi wa kituo cha polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha baada ya kukarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967 na kugharimu kiasi cha shilingi milioni 17, wakishuhudia ni Mkuu wa Kituo hicho INSP Amilton Matagi ,Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba ,Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Nguvu Kamando.
Mkuu wa Polisi Jamii wa Kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,Issaya Doya akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa VodacomTanzania Mwamvita Makamba, wakati wa sherehe ya kakabidhi rasmi kituo hicho kilichakarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Foundation kwa thamani ya shilingi Milioni 17,tangu kijengwe mwaka 1967.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC) Thobiasi Andengenye akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wakati wa hafla ya kukabidhiwa kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha , kilichokarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Tanzania kwa thamani ya Shilingi Milioni 17 tangia kijengwe mwaka 1967.katikati ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Karatu ( OCD ) Mathias Nyange.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo cha Polisi Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangia kijengwe mwaka 1967,kwa gharama ya shilingi milioni 17.Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye na kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya kaskazin Nguvu Kamando.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad