RAIS KIKWETE AWASILI GHABERONE, BOTSWANA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 24 February 2012

RAIS KIKWETE AWASILI GHABERONE, BOTSWANA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Botswana Seretse Khama wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Sir Seretse Khama jijini Gaberone, Botswana, leo February 24, 2012 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, ambapo pia atahudhuria katika sherehe za miaka 50 ya chama tawala cha BOTSWANA DEMOCRATIC PARTY kinachotawala nchini humo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na mwenyeji wake Rais wa Botswana Seretse Khama mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sir Serese Khama jijini Gaberone.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na mwenyeji wake Rais wa Botswana Seretse Khama wakiangalia ngoma ya makhirikhiri ya Botswana.
Wananchi wa Botswana akipeperusha bendera kama ishara ya makaribisho kwa Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wa Botswana mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sir Seretse Khama jijini Gaberone.

Rais Jakaya Kikwete akikagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na mwenyeji wake Rais Seretse Khama wa Botswana.  (PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment