RAIS AKABIDHI MSAADA WA NG'OMBE KWA WATU JAMII YA WAMASAI MKOANI ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


24 Feb 2012

RAIS AKABIDHI MSAADA WA NG'OMBE KWA WATU JAMII YA WAMASAI MKOANI ARUSHA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete akiwa nawasalimia wamama wa kimasai waliohudhuria kwenye sherehe hizo
Supai Kikwete!!!!wanaonekana wakisema hawa wazee wa jamii ya wafugaji...kuwa haujambo kikwete..??
 Hapa anawasalimia malaigwanani wa longido
 akiwa amekaa kwenye kiti cha kimasai cha asili kijulikanacho kwa jina la kimasai Olorika...huku akiwa amevishwa shuka ya kimasai na fimbo kama ishara ya kumpa Heshima kama raisi wa Nchi hii.

Hizi ni baadhi ya picha za sherehe ya kukabidhi ng'ombe kwa jamii ya wamaasai ,kufidia ng'ombe waliokufa wakati wa ukame, makabidhiano hayo yalifanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete.

RAIS Jakaya Kikwete  alizindua mradi wa uwezeshaji wafugaji wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha ikiwa ni kifuta jasho cha ukame uliozikumba kaya za wilaya hizo mwaka 2008 na 2009.
Wilaya zilizonufaika na mradi huo ni Longido, Monduli na Ngorongoro. Mradi huo umegharimu zaidi ya Sh bilioni 11.2 kwa wilaya hizo zilizokumbwa na ukame mkubwa uliofanya mifugo mingi kufa katika miaka hiyo hasa Wilaya ya Longido yenye tarafa nne za Ketumbeine, Enduimet, Longido na Engarenaibor.

Kabla ya ukame huo, Longido ilikuwa na mifugo 1,016,313 na baada ya ukame ikabakiwa na mifugo 555,613.
Katika sherehe zilizofanyika jana wilayani Longido na kuhudhuriwa na mamia ya watu, Rais Kikwete alisema alipotembelea wilaya hiyo Agosti 23, 2009, alijionea mwenyewe hali mbaya ya ukame iliyosababisha maisha ya watu wa wilaya kuwa magumu kwani asilimia 95 ya wakazi wa wilaya hiyo hutegemea mifugo. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad