RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA TBC MAREHEMU HALIMA MCHUKA JANA. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 31 December 2011

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA TBC MAREHEMU HALIMA MCHUKA JANA.

Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa TBC Bw Clement Mshana wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mtangazaji Halim Mchuka leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kabla ya kwwenda kuzikwa makaburi ya Msasani baada ya Sala ya Ijumaa. 
Rais Dk. Jakaya Kikwete pamona na baadhi ya ndugu na watoto wa marehemu wakiuombea dua mwili wa marehemu Halima Mchuka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka aliyefariki tarehe 29 Desemba mwaka huu jijini Dar es salaam. Mwili wa marehemu umezikwa leo katika makaburi ya Msasani jijini Dar es salaam. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo wakitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka wakiongozwa na Naibu waziri wa wizara hiyo Dkt. Fennela Mukangara (wa kwanza kulia) katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiwafariji ndugu na watoto wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka mara baada ya kuwasili katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam. 
Baadhi ya wanataaluma wa tasnia ya habari nchini na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakiwa na majonzi mara baada ya kuuaga mwili wa marehemu Halima Mchuka aliyekuwa mtangazaji wa shirika hilo kwa takribani miaka 19 leo jijini Dar es salaam. 
Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa TBC Halima Mchuka ukiwekwa katika makao ya kudumu katika makaburi ya Msasani leo jijini Dar es salaam. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki mazishi ya aliyekuwa mtangazaji wa TBC marehemu Halima Mchuka leo jijini Dar es salaam katika makaburi ya Msasani. 
(Picha na Aron Msigwa -Maelezo)

No comments:

Post a Comment