Laurent Gbagbo kufika mbele ya ICC - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 5 December 2011

Laurent Gbagbo kufika mbele ya ICC

Laurent Gbagbo kushtakiwa na uhalifu wa kivita 

Rais aliyeondolewa madarakani nchini Ivory Coast Laurent Gbagbo anafikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC hii leo. Mwansiasa huyo anatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kivita. Gbagbo alipelekewa nchini Uholanzi wiki jana.
Mahakama ya ICC imemtuhumu Gbagbo kwa makosa ya uhalifu wa kivita kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa Ivory Coast mwaka jana alipopinga kuyakabidhi madaraka kwa mpinzani wake,Alassane Ouattara, ambaye sasa ndiye rais wa Ivory Coast.
Kiongozi huyo ambaye ndiye rais wa kwanza kufikishwa mbele ya ICC atasomewa makosa yake chini ya sheria za mkataka wa Roma uliounda mahakama hiyo. Baada ya kusomewa mashtaka yake itakuwa jukumu la majaji waandamizi kuamua siku ya kusikizwa kwa kesi dhidi ya Laurent Gbagbo.

Nchini Ivory Coast wafuasi wa Gbagbo wametaja hatua ya kumkamata mwanasiasa huyo kama utekaji nyara wa kisiasa na kuonya hatua ya kumfungulia mashataka inahujumu mpango wa maridhiano ya kitaifa. Hata hivyo Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya ya ICC anayeondoka Luis Moreno Ocampo amekanusha kauli hiyo na kusema kuna ushahidi tosha kumfungulia kiongozi huyo mashkata ya uhalifu wa kivita na siyo shinikizo za kisiasa.
Mahakama ya kimataifa ya jinai ilianzishwa mwaka wa 2002. Hii ndiyo kesi ya kwanza kubwa kusikilizwa katika mahakama hiyo.Baadhi wadadisi wameona kama ushindi kwa mahakama hiyo huku baadhi nao wakiendelea kulalalamikia utaratibu wa pole hususan katika utekelezwaji wa kesi. Kuna wengine ambao wamelalamikia mahakama ya ICC kwa kuwalenga viongozi na wanasiasa wa bara Afrika Pekee na kufungia macho mataifa mengine hasa ya magharibi.

No comments:

Post a Comment