NBC YASHEHEREKEA SIKU YA WANAFAMILIA SOUTH BEACH.. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 5 December 2011

NBC YASHEHEREKEA SIKU YA WANAFAMILIA SOUTH BEACH..

Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa benki ya NBC wakishindana katika mbio za magunia katika Siku ya Wanafamilia ya benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam jana. Robert Kusekwa (wa pili kulia) alibuka kidedea.
Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa benki ya NBC wakishindana katika kuvuta kamba ili kumpata mshindi katika Siku ya wanafamilia ya benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa benki ya NBC wakishindana katika mchezo wa kufukuza kuku katika Siku ya Wanafamilia ya benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam. Mshindi wa mbio hizo huondoka na kuku huyo na kwenda nae kumfanya kitoweo au kumfuga.
Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa benki ya NBC wakifurahi katika bwawa la kuogelea ikiwa ni baadhi ya burudani kuadhimisha Siku ya Wanafamilia ya benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kushoto) akishiriki kusakata dansi lililokuwa likiporomoshwa na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ wakati wa sherehe za Siku ya Wanafamilia wa benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.
Ofisa Uhusiano wa NBC, Eddie Mhina akigawa zawadi kwa baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa sherehe za Siku ya Wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment