Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) katika Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo,Raphael Hokororo akiwapa maelezo kuhusu historia za picha za kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Viongozi mbalimbali wa kitaifa wa zamani na wale wa sasa kwa wanafunzi wa shule ya awali na msingi ya Mbeza iliyopo kijijini Butiama, mkoani Mara mara baada ya kutembelea banda la Idara hiyo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa Wizara hiyo. Katikati ni mwalimu wa wanafunzi hao Emelda Mutua.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Raphael Hokororo akimpa maelezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda mara baada ya kulitembelea banda la idara hiyo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa Wizara hiyo yanayoendelea katika viwanja vya Joseph Kazurira Nyerere huko Butiama, mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara akimpatia kitabu cha taarifa ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara kwa Wizara hiyo leo nyumbani kwa Mjane wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake Butiama, mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara mara baada ya kumtembelea Mjane wa Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere kijijini kwake Butiama, mkoani Mara leo. Wengine katika picha ni Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo, kulia hiyo ni mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere.
Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Charles Makongoro Nyerere akitoa historia ya makaburi ya wazazi wa mwalimu Julius Nyerere yaliyopo mwitongo, Butiama kwa Viongozi waandimizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waliokwenda kumjulia hali Mama Maria Nyerere.
Mkuu wa mkoa wa Mara John Tupa(katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika banda la Idara ya Habari kuhusiana na maandalizi ya mbio za mwenge wa uhuru unaotarajia kuwashwa mkoani humo. Wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga na kwanza na kwanza kushoto ni kaimu Afisa Utamaduni na Michezo, Shekheadi Saidi. Wengine wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Clement Lujaji na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Karaine Kimaati.
picha na Full shangwe Blog
No comments:
Post a Comment