TAMASHA LA SERENGETI FIESTA LAWASHA MOTO UWANJA WA USHIRIKA USIKU HUU - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 16 July 2011

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA LAWASHA MOTO UWANJA WA USHIRIKA USIKU HUU

Kundi la Nako2Nako likifanya vitu vyake jukwaani katika Mwendelezo wa tamasha la msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta, linaloendelea usiku huu kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi, kuna umati mkubwa wamashabiki waliojitokeza ili kushuhudia tamasha hilo, na wasanii wanaendelea kutoa burudani ya kutosha muda wote ni nderemo na vifijo watu wakishangilia wasanii mbalimbali wanaopanda jukwaani na kuimba.
Mkurugenzi wa G5Click Mustafa Selemani kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Clouds Entarteinment Joseph Kussaga.
Nako2Nako wakiendeleza raha jukwaani.
Mashabiki wakishangweka na Serengeti Fiesta mjini Moshi usiku huu.
Huyu anaonekana akiruka kwa nguvu juu baada ya Majotroo ya Fiesta kumpanda.
Kulia ni Chege Chigunda na Mh. Temba kutoka kundi la TMK wakipagawisha mashabiki.
Ulinzi umeimarishwa ili kuhakikisha usalama katika tamasha hilo la Serengeti Fiesta.
Hapa ni Habari Zeeenyu baaaana.
Umati unashindwa kuvumilia na unaonekana wenye kufurahia kupita kiasi tamasha hilo kama unavyoona
Kundi la TMK liendelea kushabulia jukwaa.
picha na full shangwe blog:

No comments:

Post a Comment