Chi..chi..Chid Benz ....msanii machachari kutoka kundi La Familia Pande za Ilala,akifanya mambo makubwa katika katika jukwaa la Mwendelezo wa Msimu wa dhahabu na Serengeti Fiesta tamasha la pili katika mikoa ya kanda ya Kaskazini, baada ya lile la mjini Moshi jana ambalo lilifana sana na kukusanya mashabiki lukuki. Tamasha la Serengeti Fiesta jijini Arusha limehudhuriwa na umati wa mashabiki.
Kwa mbali linaonekana jukwaa likiwa limezingirwa na mashabiki wakishuhudia burudani mbalimbali inayotolewa na wasanii mbalimbali katika tamasha hilo.
KIjana mkali kutoka jijini Mbeya Godzilla akighani jukwaani wakati wa tamasha kubwa la Serengeti Fiesta linalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Kundi la Contagious(Arusha Boys Crew) lililoshinda katika mashindano ya Serengeti Dansi la Fiesta likitumbuiza katika tamasha la Serengeti Fiesta Arusha.
Wadau hawa hawakukosa katika tamasha la Serengeti Fiesta jijini Arusha kutoka kulia ni Getu, Recho,Phide na Marystela.
Msanii wa muziki wa muziki wa bongofleva Diamond akiimba na kundi lake katika jukwaa , mwanamuziki huyo alivutia mashabiki wengi kutokana na staili yake anayotumia katika kucheza na kundi lake, lakini pia unadhifu wa mwanamuziki huyo na kundi lake.
Diamond pia ana uwezo mzuri wa kucheza kama unavyomupona akienda sambamba na wanengiuaji wake kama wanavyoonekana wakiwa nadhifu kwa mavazi yao pia.
Diamond haumwi tumbo ila ni staili tu za uchezaji wake akiwapa mashabiki wake Majotroo ya Serengeti Fiesta.
Rachel msanii chipukizi wa muziki wa bongofleva kutoka kundi la THT akiimba na kumwaga mauno jukwaani jioni hii
Rachel Msanii chipukizi kutoka kundi la THT naye amefanya mambo makubwa jukwaani kama unavyomuona kinyonga viuno.
Wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya tayari wameshaanza kupanda jukwaani kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, na kufanya vitu vyao huku wakionyesha uwezo mkubwa,
Umati mkubwa umefurika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kama unavyoonekana katika picha.
Huyu ni mmoja wa wasanii chipukizi mkoani Arusha ameimba kwa uwezo mkubwa na kushawishi umati uliokuwa ukimuangalia.
Binamu MwanaFA kushoto akiwa amepozi kwa picha na wasanii wenzake kabla ya kupanda jukwaani rasmi. Mkurugenzi alikutana na mmoja wa Funs wa FULLSHANGWEBLOG Upendo wakapiga picha kwa kumbukumbu
Hawa ni (Diamond Boy) wacheza shoo wa msanii Daiamond wakiwa tayari kwa kutoa burudani katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha jioni hii.
picha zote na:fullshangwe blog
No comments:
Post a Comment