Wakiongea na waandishi wa habari madereva hao wamesema kuwa wameamua kufikia uamuzi huo kutokana na kunyanyaswa na askari wa bara barani kila mara kwani wamekuwa wakiwakamata na kuwapeleka polisi bila ya kuwa na kosa lolote.
Walisema kuwa tatizo hilo wameanza kulipata juzi ambapo kwa ziku iyo zaidi ya madereva 17 walikamatwa bila ya kuwa na kosa lolote hali ambayo inawafanya hadi hao wenyewe kushindea kufanya kazi kwa amani.
Mmoja wa madereva hao aliyejitaja kwa jina la Saidi Ally alisema kuwa wamekuwa wakipata msuko suko huo bila ya kujua sababu yeyote hivyo wameamua kugoma mpaka pale ambapo watakapo ambiwa sababu ya wao kukamatwa na kutofanyiwa hivyo tena.
"unajua sisi tumekuwa tukikamatwa ovyo bila ya kupewa sababu yeyote na maaskari na baada ya kutukamata wamekuwa wanatuambia tuwape shilingi laki moja na iwapo mtu akimwambia hana au baadae basi anachukuliwa na kupelekwa polisi na kuwekwa lokapu na akishawekwa huko haruhusiwi kupewa mzamana sasa jamani sawa wametukamata kwani sisi ni majambazi au wauaji mpaka mtu ukikamatwa unyimwe mzamana"alisema Hamisi.
Alibainisha kuwa mpaka kufikia leo zaidi ya madereva 29 wamekamatwa na wengine wameshapelekwa mahakamani huku mwenzao mmoja akiwa amekamatwa na kubambikiwa kesi ya roba.
kwa upande wa dereva munguine aliyejulikana kwa jina la Mfundo Hassan alisema kuwa tatizo hilo limewatatiza na wameshapeleka malalamiko yao hadi kwa mkuu wa usalama barabarani lakini hawajapata ufumbuzi kwani hawajasaidiwa kitu chochote.
Walisema kuwa wataendelea kugoma mpaka pale watakapo jua sababu haswa ya wao kukamatwa na kupelekwa mahakamani bila ya kuwa na sababu yeyote .
'sisi tutagoma mpaka pale tutakapo tambua sababu haswa ya askari hawa kutukamata kwani kama ni makosa ya barabarani si watuambie ili tujue na kama basi ni makosa kwani sikuna faini watuambie tulipe faini tuendelee na sio kama wanavyofanya wanatukamata afu wanamuita tajiri achukue gari afu sisi wanatupeleka magereza"alisema Mfundo
Libeneke lilizungumza na baadhi ya abiria ambao walionekana kutembea kwa miguu na wengine walikuwa wakitafuta usafiri nao walisema kuwa wanawaomba askari wawaache madereva hawa wafanye kazi kwani wamekuwa wanapata shida sana.
Mmoja aliyejitambulisha kwa jina la mama Zaina alisema kuwa yeye mwenyewe anasikitika kwani asubuhi mtoto wake alitelekezwa njiani na gari ya shule kutokana na dereva wa gari hilo kukimbia askari mara baada ya kuwaona.
"unajua watoto wetu leo wametelekezwa na dereva kutokana na kukimbia askari hawa wanaokamata madereva wa daladala kwani dereva huyu alikuwa amebeba wanafunzi wadogo wa miaka minne wengine mitano na hata mitatu sasa alivyofika mbele akaona askari ilibidi asimamishe gari afu akimbie aache watoto wale njiani kweli jambani ni haki kweli naomba waache basi ili tuweze kuipata usafiri mzuri bila ya wasiwasi"alisema mama huyo
Alisema kuwa iwapo vijana hawa wanaoendesha daladala wakinyimwa kufanya kazi hizi si wezi utaongezeka mjini hivyo aliwasihi maaskari hao kuacha kufanya ivyo na badala yake kukamata magari ambayo yanamakosa na kuyafikisha polisi na wakikutwa na kosa la kawaidi basi wapige faini na kama ni kubwa basi wawapeleke mahakamani na sio kuwakamata tu bila ya kuwa na sababu.
libeneke halikuishia hapo lilimfata kamanda wa usalama barabarani Nestory Didi naye alisema kuwa ni kweli wanakamata madereva hao na sio kwa kutokuwa na kosa bali wanawakamata kutokana na kukiuka sheria za usalama barabarani.
Alisema kuwa watu hao wamekamatwa na kufikishwa mahakamani mara baada ya kitengo chao cha usalama barabarani kuanzisha uperesheni maalumu kwa ajili ya kuwakamata madereva wanaokiuka sheria za bara barani.
Alibainisha kuwa operetioni hiyo ilianza wiki iliyopita na walianzia katika barabara ya mbauda na kunamadereva ambao walikamatwa na wamefikishwa mahakamani kutokanana makosa mbalimbali wanayoyafanya wanapokuwa barabarani.
"unajua kwanza katika barabara hii ya ungalimitedi magari mengi ni mabovu madereva wengi wanaendesha magari bila ya kuwa na leseni hawana leseni ya usafirishaji hivyo tumekamata watu kwa makosa mbalimbali sasa wanavyosema kuwa wanakamatwa kwa kosa la kutofuata sheria kweli hapo ni uongo"alisema Didi
Aliongeza kuwa swala la askari kupokea shilingi laki moja hilo si alijui na anathani sio kweli kwani iwapo mtu akikamatwa kwanini anatoa hela si aache kutoa ela na aende afuate sheria .
"kwa swala hili la uyu dereva ambaye wanadai kabambiokiwa kesi ya wizi sio kweli kwani dereva huyu kaja apa na tumemshika kuokana na anadaiwa kujiusisha na kazi ya ujambazi na tutamfikisha mahakamani pindi tutakapo maliza upelelezi'alisema Didi
Aliongeza kuwa wao kama jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wataendelea kukamata watu ambao wanakiuka sheria za usalama barabarani na watawafikisha mahakamani hadi pale ambapo wataacha kukiuka sheria za barabarani.
"sasa nataka kumalizia kwa kusema kuwa madereva na abiria kwa ujumla watii sheria bila ya kushurutishwa iwapo watafanya hivyo usumbufu hautata tokea na iwapo hawatatii sheria basi itabidi washurutishwa"alisema Didi.
by: libeneke la kaskazini
No comments:
Post a Comment