JAKAYA KIKWETE NA DKT BILAL WAHUDHURIA NDOA YA YUSUPH KIKWETE BAGAMOYO LEO - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 16 July 2011

JAKAYA KIKWETE NA DKT BILAL WAHUDHURIA NDOA YA YUSUPH KIKWETE BAGAMOYO LEO

Rais jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt Mohammed Gharib Bilal, wakiongozana katika Uwanja vya Ikulu Ndogo Bagamoyo wakati walipofika kuhudhuria sherehe ya ndoa ya mdogo wake na rais Kikwete, Yusuph Kikwete, iliyofungwa leo mchana katika uwanja huo na kuhudhuriwa na mbalimbali pamoja na wake za viongozi.
Rais Jakaya, akifurahia jambo na Mama Zakhia Bilal (kushoto) na Mam Asha Bilal (wapili kulia)
Bwana Harusi, Yusuph, akifungishwa ndoa na Sheikh
Bwana Harusi Yusuph na waumini wa dini ya Kiislamu wakiomba dua baada ya tendo la kufungishwa ndoa.
Sheikh, akitoa mawaidha baada ya bwana harusi kufungishwa ndoa,
Bwana Harusi, Yusuph Kikwete akiwa na mkewe Mariam Ombaka, baada ya kufungishwa ndoa.
Mama Salma Kikwete (kushoto) akiwa na Mama Zakhia Bilal (katikati) na Mama Asha Bilal, wakati wakiwa katika sherehe hiyo ya ndoa ya mdogo wake na Rais Jakaya Kikwete, Yusuph Kikwete leo mjini Bagamoyo.
Rais jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete na Bwana na Bi Harusi.
 
fullshangwe blog

No comments:

Post a Comment