Matukio : Sijaridhishwa na Ujenzi wa Kituo cha Sirari - Majaliwa - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


18 Jan 2018

Matukio : Sijaridhishwa na Ujenzi wa Kituo cha Sirari - Majaliwa


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ubora wa ujenzi wa kituo cha forodha cha Sirari kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.


Kufuatia hali hiyo amemtaka Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) afike ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma akiwa na mkandarasi aliyejenga kituo hicho.“Serikali haiwezi kuvumilia ujenzi wa hovyo kiasi hiki, namtaka Kamishna wa TRA aje ofisini kwangu Januari 25, 2018 pamoja na mkandarasi aliyejenga kituo hiki akiwa na nyaraka zote za ujenzi wa jengo hilo.”


Ameyasema hayo leo (Jumatano, Januari 17, 2018) mara baada ya kumaliza kukagua kituo hicho kilichopo wilayani Tarime, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mara.Waziri Mkuu amesema hajaridhishwa na ujenzi huo kwa kuwa upo chini ya kiwango. Kituo hicho kilianza kujengwa mwaka 2011 na kukamilika mwaka 2014.


Waziri Mkuu amejionea mwenyewe kuta za jengo hilo zikiwa na nyufa nyingi kuanzia ukutani hadi sakafuni na pia rangi za baadhi ya kuta zikiwa zimebanduka.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wananchi wa wilaya hiyo kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa kuzingatia sheria na wajiepusha na biashara za magendo.


Waziri Mkuu amesema magendo yanaikosesha Serikali mapato, hivyo bidhaa yoyote itakayokamatwa ikiingizwa nchini kwa njia za magendo itataifishwa pamoja na chombo cha usafiri kilichotumika. Pia Waziri Mkuu ametembelea shule ya Sekondari ya Wasichana ya Borega, ambapo amewasisiza wananchi wasimamie elimu ya watoto wa kike ili wafikie malengo yao.


Amesema Serikali imeweka sheria kali kwa yeyote atakayekatisha masomo kwa watoto wa kike iwe kwa kumpa ujauzito au kumoa, adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela. Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka wanafunzi hao wasome kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao na kamwe wasijihusishe katika mambo ambayo hayahusiani na masomo.




IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, JANUARI 17, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimu wagonjwa wakati alipotembela hospitali ya wilaya ya Tarime akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 17, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adm Malima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mtoto Naomi Ogaja (3) aliyelazwa katika hospitali ya walaya ya arime kwa matibabu wakati alipotembelea hospitali hiyo Januari 17, 2017. Kshoto ni baba mzazi wa mtoto huyo Ogaja Wajangwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Sirari na kueleza kutorihishwa kwake na viwango vya ujenzi wa jengo hilo (pichani) ambalo limeanza kuharibika Januari 17, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adama Malima. (Picha na Ofisi Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Sirari na kueleza kutorihishwa kwake na viwango vya ujenzi wa jengo hilo (pichani) ambalo limeanza kuharibika Januari 17, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Sirari wilayani Tarime Januari 17, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Boreha wilayani Tarime, Januari 17, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maeneo na majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Borega wilayani Tarime baada ya kuifungua akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara Januari 17, 2018.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad