MATUKIO : UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON, DC WAMKARIBISHA BALOZI OMBENI SEFUE KWA CHAKULA CHA JIONI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


9 Oct 2014

MATUKIO : UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON, DC WAMKARIBISHA BALOZI OMBENI SEFUE KWA CHAKULA CHA JIONI


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwasili kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC nchini Marekani alikokaribishwa chakula cha jioni wakiwemo viongozi mbalimbali wa Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania. Mhe. Ombeni Sefue ndiye aliyewezesha ununuzi wa jengo hilo la Ubalozi wakati alipokua Balozi wa Tanzania nchini Marekani mwaka 2007
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akimpokea Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue siku ya Jumatano Oct 8, 2014 siku Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ulipomkaribisha chakula cha jioni wakiwemo viongozi mbalimbali wa Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea mawili matatu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile.
Mhe. Liberata Mulamula akimkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na kumshukuru kwa kuwezesha upatikanaji wa jengo hilo la Ubalozi.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akimshukuru Balozi Liberata Mulamula na kuelezea ununuzi wa Jengo hilo ulivyofanyika yakiwemo majengo mengine ya Ubalozi Canada na New York huku akisema ni jambo jema kwa Serikali kuangalia uwezekano wa kununua majengo ya Ubalozi na makazi ya maafisa wake badala ya kukodisha kwani kufanya hivyo kunapunguza gharama kwa kiasi kikubwa sana yeye aliliona hilo ndio maana alipendekeza na hatimae kuwezesha ununuzi wa majengo hayo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akijichukuli chakula.
Wageni wakiendelea kupata chakula cha jioni. Picha na Vijimambo Blog.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad